Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko amewaomba wananchi wa
Jimbo lake kuwa na Imani naye kwani yeye ndiye mwakilishi wao kwa sasa
huku akiwaomba na kuwasihi wazidi kumuombea Rais Magufuli kwa kazi ngumu
anayoifanya ya kuwatetea wanyonge pamoja na maslahi ya Taifa kwa ujumla.
Biteko amebainisha hayo katika mkutano wake wa kuwashukuru wananchi wa
Jimbo hilo la Bukombe kwa kumuwezesha kumchagua kwa kura nyingi na pia
kumpigia Rais Magufuli kwa kula za kutosha kuingia madarakani.Aidha,Doto aliwaomba wananchi wa Kata Bulangwa kuwa na subira kwani atahakikisha Umeme wa gridi ya Taifa inapita katika vijiji vyote vya Wilaya ya Bukombe uku akiwabainishia mradi uliokwisha haukua Mradi wa REA hivyo amewaeleza mpango wa sasa ni kupata umeme wa uhakika hadi kwenye baadhi ya vyanzo vya maji ili kupunguza na changamoto ya maji na kwa sasa tayari ameliombea hilo na litatekelezwa muda wowote kuanzia sasa.
Mbali na hilo pia aliwataka wananchi wa Jimbo hilo la Bukombe kutojenga katika miundo mbinu ili wakati wa serikali kufanya maendeleo kusiwe na kikwazo cha kuwaathiri wananchi hao.
Mhe. Doto Mashaka Biteko pia mbali na kutoa shukrani kwa wapiga kula wake hao, pia alipata wasaha wa kusikiliza kero za wananchi huku akipokea kero zao hizo ambapo ameeleza kuwa atazifanyia kazi
Wananchi waliuliza maswali mbalimbali ikiwemo ukosefu wa maji,kusumbuliwa na wahifadhi na kuuliza nini hatima ya serikali juu ya milioni hamsini za kila kijiji, barabara mbovu pamoja na Ukosefu wa Umeme.
No comments:
Post a Comment