Kaimu Mkurugenzi wa tiba na
ushauri wa kiufundi NHIF Makao makuu ,Dr Aifena Mramba akielezea malengo ya
kuwepo kwa madkatari Bingwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita wakati
wa hafra fupi ya uzinduzi ambayo imefanyika kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
huo.
Kaimu
Mkurugenzi wa tiba na ushauri wa kiufundi NHIF Makao makuu ,Dr Aifena Mramba
akimkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Celestine Gesimba Shuka mia moja
ambazo wametoa kama msaada kwa hosptali hiyo.
Meneja wa
NHIF Mkoani Geita Mathias Sweya Akitoa utambulisho mbele ya mgeni Rasmi wakati
wa Hafra fupi ya uzinduzi wa Mpango wa Madaktari Bingwa.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF) umezindua mpango wa madaktari Bingwa
Mkoani Geita lengo likiwa ni kushirikiana na serikali kupunguza
changamoto za upatikanaji wa huduma za kibingwa na kusogeza huduma karibu na
wananchi pamoja na wanachama wa mfuko huo.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo Kaimu Mkurugenzi wa tiba na ushauri wa
kiufundi NHIF Makao makuu ,Dr Aifena Mramba amesema watu elfu kumi na
tatu mia moja na sitini na saba (13167) na kati ya hao mia nne sitini(460)
wamekwisha kufanyiwa huduma ya upasuaji.
“Kabla ya kuleta madaktari bingwa kwenye Mkoa husika mfuko huwa unafanya
tathimini na kubaini uhitaji katika kila Mkoa ndivyo hivyo tumefanya kwenye
Mkoa huu wa Geita na kuamua kuleta madaktari bingwa kama ambavyo nimeeleza
kwa hiyo Tumekuja na madaktari Bingwa pamoja na Dawa na mashuka ambavyo
vitasaidia kwenye huduma za kiafya”Alisema Mramba.
Aidha Bi, Mramba ameongezea kuwa matarajio ya mfuko huo ni kupunguza
msongamano wa wagonjwa katika hospitali za ngazi ya juu ikiwa ni pamoja na
kutoa fursa kwa madaktari kutoa huduma kwa uhakika zaidi kwa watu wachache
watakaolazimika kufuata huduma hizo kwenye hospitali Kubwa ikiwa ni pamoja na
watumishi wa Hospitali husika kutumia fursa ya kujifunza kwa kupata ujunzi na
utaalamu kupitia kwa madaktari wageni.
Kwa Upande Wake Mgeni Rasmi Ambaye ni Katibu Tawala Mkoani Humo Celestine
Gesimba amewata madaktari kuwatumia madaktari bingwa waliofika
Hospitalini hapo kutoa huduma kwa wagonjwa ili kujifunza mbinu mpya za utoaji
wa huduma badala ya kwenda kufuata mbinu hizo nje ya maeneo yao ya kazi
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Watoto kutoka Hospitali ya Rufaa ya Bugando
Dr Neema Chami amesema tangu kuanza kwa huduma hizo kwa siku 2 sasa
wamewahudumia watoto 80 hali inayoonesha mafanikio ya lengo la wao kufika
mkoani humo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Geita Dr Brian Mawala amesema
ombi la Wananchi la kutaka Madaktari Bingwa wawe wanafika mara kwa mara
Hospitalini hapo, litafanyiwa kazi kupitia mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF
ili kupunguza wananchi wasisafiri umbali mrefu kufuata huduma za Kibingwa
Zoezi la utoaji wa huduma za upasuaji kutoka kwa Madaktari Bingwa
kwenye Mikoa ya Geita na Kigoma lilianza rasmi Mei 22
siku ya jumatatu kwa uratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF
ambapo hadi sasa ni jumla ya wagonjwa 1,204 wamekwisha hudumiwa kwa
siku mbili huku wagonjwa ambao wamefanyiwa upasuaji kwa mikoa miwili ni
kumi na nne.
No comments:
Post a Comment