Mkuu wa
wilaya ya Geita Mwl. Herman Kapufi akikagua shamba la mahindi kwenye
kijiji cha nyang'uku .
Mkuu wa
Wilaya akiwa na baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Geita pamoja na
madiwani wakati wa kuzungukia mashamba Kwenye vijiji vya Nyang'uku,Ibanda na
Bungwangoko.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Mji wa Geita Leornad Kiganga Bugomola akikagua Shamba la Uele
kijiji cha Nyang'uku wakati wa ziara ya kutembelea wakulima Mashamba.
Serikali ya Wilaya ya Geita ,inatarajia kujenga mradi wa Bwawa la
Maji kwaajili ya Kilimo cha umwagiliaji kwenye vijiji vya
ibanda kata ya Kanyara Chabulongo na Mkoba kata ya Bungwangoko ambapo
utaghalimu jumla ya kiasi cha Sh,Bilioni mbili na nusu.
Akizungumza na Maduka online ,Fundi Sanifu umwagiliaji wa
Halmashauri ya Mji wa Geita,Ally Semfukwe,amesema kuwa mradi ambao unatarajia
kujengwa utanufaisha vijiji vitano ambapo viwili vinatoka kwenye
Halmashauri ya wilaya ya Sengerema na vingine vitatu kwenye wilaya ya Geita.
“Mradi huu wa Bwawa la maji naamini wakulima wataweza kufaidika nao kwani
ni shughuli nyingi ambazo watakuwa wakizifanya tukiachana na Kilimo wanaweza
kutumia pia kwaajili kunyweshea mifugo na kwamba kukamilika kwa mradi huo utaghalimu
kiasi cha sh,Bilioni mbili na nusu”Alisema Semfukwe.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Modest Aporinali amebainisha
kuwa eneo ambalo litatumika kwaajili ya shughuli za utengenezaji wa
Bwawa hilo ni zaidi ya Hekari 500 hadi 1000 na kwamba maeneo hayo ni makazi ya
watu na mradi huo ni wa serikali kuu ambapo wataangalia ni maeneo gani ambayo
ni makazi ya watu kwaajili ya kuwalipa fidia wale ambao watakuwa wamefikiwa na
mradi.
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi amezungumza na wananchi wa
kijiji chA Ibanda kata ya Kanyara wakati wa ziara yake ya kuzungukia kwenye
kata ya Nyang’uku,Kasamwa ,Bungwangoko na Kanyara ambayo ilikuwa na lengo la
kuangalia kilimo cha Mtama,Mhogo pamoja na pamba,wananchi hao mradio huo
ukikamilika utaleta faida kwani awatakuwa wa kusubilia Msimu wa Mvua na kwamba
maji yatapatikana muda wote pindi wanapoitaji kufanya shughuli za kilimo.
Hata hivyo pamoja na Mradi huo kuwa ni wamanufaa kwa wakulima ,baadhi ya
wakulima wa kijiji cha Ibanda wamepinga Hatua hiyo na kusema kuwa wao
wameshazoea kilimo cha zamani na kwamba yawezekana kisiwe na tija kwao kutokana
na kwamba wanaweza wakajikuta wakilipia ghalama za kunyweshea mifugo yao.
Mradi wa umwagiliaji kama utakamilika unatarajia kuwanufaisha zaidi ya
wananchi laki moja kutoka kwenye vijiji vitano.
No comments:
Post a Comment