Serikali kupitia
Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi,na Mawasiliano imetenga Shilingi bilioni
thelathini(30) katika mwaka wa fedha 2017/2018 ili kukamilisha malipo ya fidia
kwa wananchi wa Kipunguni wanaopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege.
Hayo yamesemwa leo na
Naibu Waziri wa Ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani Bungeni
Mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Segerea Mhe.Bonnah Kaluwa.
“Ni kweli Serikali
ilifanya uthamini wa mali za wananchi ili kupisha upanuzi wa kiwanja cha Ndege
cha Kimataifa cha Dar es Salaam mwishoni wa miaka ya 90 ambapo maeneo
yaliyoainishwa kwa ajili ya upanuzi huo ni Kipawa,Kigilagila na
Kipunguni”,Alisema Mhe.Ngonyani
Ameongeza kuwa
kutokana na gharama za fidia na uhaba wa fedha,Serikali imekuwa ikilipa fidia
kwa wakazi hao kwa awamu.
Ambapo Mwaka 2009/10
wakazi wapatao 1500 wa eneo la Kipawa walilipwa fidia zinazofikia
shilingi bilioni 18 ambapo zoezi hilo lilikamilika Januari 2010.
Katika mwaka wa Fedha
2010/2011 Serikali ililipa Shilingi Bilioni 12 za fidia kwa wakazi 864 wa
Kigilagila na Malipo yalikamilika Januari 2011.
Katika mwaka 2013/14
Serikali ililipa Shilingi Bilioni 1.2 ikiwa ni fidia kwa wakazi 59 kati ya
wakazi 801 kwa eneo la Kipunguni.
Aidha katika malipo
hayo ni wakazi 742 wa Kipunguni ndio ambao hawajalipwa fidia zao zenye thamani
ya takribani 19.
“Mwaka
wa Fedha 2016/17 Serikali imetenga Shilingi Bilioni tano kwa ajili ya kulipa
fidia kwa wakazi hao wa Kipunguni”Alisisitiza Mhe.Ngonyani.
No comments:
Post a Comment