Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl. Herman Kapufi amewataka wanasheria kuwasaidia
wananchi kujua elimu ya sheria kutokana na wengi wao kushindwa kujua sheria
hali ambayo inasababisha wengi kukosa haki zao za msingi pindi wanapofuatilia
haki zao.
Hayo ameyasema wakati akifungua Taasisi isiyo ya kiserikali ya msaada wa
kisheria ya “Himiza Social Justice” Wilayani hapa amesema elimu ya sheria
na ushauri ni muhimu sana na kwamba kesi za migogoro ya ardhi mirathi,
kesi za jinai na madai ni nyingi kutokana na wengi kutokujua kesi hizo wanaweza
kuzipeleka sehemu gani kwa ajili ya msaada.
Watu wengi ambao wamekuwa wakikwama kesi zao wamekuwa wakikimbilia kwenye
ofisi ya mkuu wa Wilaya jambo ambalo ni ngumu kwa Mkuu wa Wilaya kuingilia
kwani Mahakama ni chombo huru kisichoingiliwa na muhimili wowote ule .
“Mahakama ni muhimili ulio huru
kumejengeka desturi ya baadhi ya wananchi Wilayani hapa kuja ofisini kwangu
kuomba msaada wa kisheria jambo ambalo sio sahihi natoa Wito kwa wananchi
kutambua kuwa huwezi kuingilia muhimili huu ni vyema wakawaoana wanasheria na
mahakimu kwa msaada zaidi”Alisema Kapufi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi hiyo,Bernad Otieno,ameelezea kuwa
kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni kutokana na kuwepo kwa tatizo la
msaada wa kisheria hususani kwa watu wasiojiweza ikiwa ni pamoja na
upungufu wa mawakili kwa maeneo ya vijijini.
“Vijana wachache Nikiwemo Mimi ,waliamua
kuanzisha shirika hili walitamani na wanatamani kuongeza ubora wa upatikanaji
wa haki katika jamii kupitia utoaji wa msaada wa kisheria ,ujenzi wa uwezo
kwenye mambo ya kisheria na haki za biashara”Alisema Otieno.
Otieno aliongeza kuwa hadi Mwaka jana Tanzania Ilikuwa na sheria ya
upande mmoja ya utoaji wa msaada wa kisheria iliyokuwa inajulikana kama The
legal Aid(Criminal Proceesings)Act Cap.21(Kabla haijafutwa) ambayo kwa kiasi
kikubwa ilikuwa ikisaidia utoaji wa msaada wa kisheria kwa kiasi kikubwa kwa
watu wenye makosa ya mauaji ,sheria ambayo inatoa nafasi kwa watu wengine
wanaoshitakiwa kwa makosa ya jinai kupata msaada wa kisheria.
“Huu ndiyo ulikuwa msukumo Mkubwa wa kuhakikisha
jamii kubwa ya watu wa Geita na Tanzania Kwa ujumla hawawezi kumudu gharama za
uwakilishi mahakamani na hata za kumuajiri wakili kwa shunghuli zao za kisheria” Aliongezea Otieno.
Hata hivyo baadhi ya wananchi Wilayani Humo,Eva Alex na Getruda Alias
wamesema kufunguliwa kwa ofisi hiyo itatoa msaada mkubwa wa kisheria kwani ni
muda mrefu wananchi wamekuwa wakikosa haki zao za msingi kutokana na kutokujua
sheria hivyo ofisi hiyo itakuwa mwarobaini wa matatizo ya kisheria.
No comments:
Post a Comment