Serikali kupitia
Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na Watoto imesema kuwa hali ya
upatikanaji wa Dawa nchini imeimarika na kufikia asilimia 83.
Hayo yamesemwa na
Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Khamis Kigwagalla alipokuwa akijibu Hoja
mbalimbali za Wabunge leo Mjini Dodoma.
“Moja ya vipaumbele
vya Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa John Pombe Magufuli ni
kuboresha upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya vya umma
nchini”Alisema Mhe.Kigwangalla.
Amesema kuwa katika
kutekeleza azma hii Serikali ilichukua juhudi za makusudi kwa kuongeza bajeti
ya dawa kutoka bilioni 31 katika mwaka wa fedha 2015/16 hadi kufikia bilioni
251,500,000,000 katika mwaka wa fedha 2016/17.
Aidha hadi kufikia
Mwezi April 2017 Jumla ya Bilioni 112 zilikwisha kutolewa na kupelekwa Bohari
ya Dawa ili kuviwezesha vituo vya kutolewa huduma za Afya vya Umma kupata
mahitaji yake ya Dawa,Vifaa,Vifaa tiba na Vitendanishi.
Kufuatia Ongezeko ilo
la fedha kumbukumbu zinaonyesha kuwa hali ya upatikanaji wa dawa nchini
imeimarika sana.
“Hadi kufikia tarehe
15 Januari 2017,Mkoa wa Kagera pekee umepokea kiasi cha bilioni 4,150,767,216
kupitia fungu 52 kwa ajili ya kununulia dawa,vifaa,vifaa tiba na
vitendanishi.”Aliongeza Mhe.Kingwangalla.
No comments:
Post a Comment