Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akikabidhi
vitambulisho vya watumishi kwa mwakilishi kutoka wilaya ya Mbongwe Bw,Paul
Cheyo wakati wa zoezi la uzinduzi wa vitambulisho vya Taifa Mkoani Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Meja jenerali Mstaafu
Ezekiel Kyunga,akionesha kitambulisho chake baada ya kukabidhiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga amewataka
watendaji kusimamia kwa umakini zoezi la vitambulisho vya Taifa litakapoanza
ili kuakikisha kila mwananchi anapata kitambulisho hicho lengo ni kujua na
kuwatambua wananchi ambao wapo Mkoani humo.
Hayo ameyasema wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa
vitambulisho vya Taifa(NIDA) lililokuwa linaambatana na utoaji wa
vitambulisho kwa watumishi wa serikali.
Kyunga amewataka wananchi kuwa na ushirikiano kufanikisha zoezi hilo
ambalo linatarajia kuanza mwezi January mwakani baada ya kuwa
limemalizika kwa watumishi wa serikali Mkoani Humo.
Ameeleza kuwa shughuli ya uandikishaji wa vitambulisho hivyo utasaidia
kujua ni idadi ya wananchi wangapi ambao wapo kwenye Mkoa wa Geita
lakini pia katika kata,mitaa na vitongoji.
Pia amewaasa wale ambao sio watanzania lakini wapo Mkoani kwa
shughuli mbali mbali zikiwemo za uwekezaji kuacha kujiingiza kwenye
usajili huo na badala yake wasubilie taratibu ambazo zitatangazwa na tume
ya Taifa vitambulisho vya uraia.
No comments:
Post a Comment