Zaidi ya mabasi 70 ya
daladala yanayosafirisha abiria katika baadhi ya njia za manispaa ya Dodoma,
yamegoma kutoa huduma kwa siku nzima ya leo kutokana na madai ya kunyanyaswa na
askari wa usalama barabarani.
Daladala hizo
zinazotoa huduma kati ya Jamatini na Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) pamoja na
Jamatini na Veyula, zilisimamisha huduma zake kwa siku nzima ya leo zikipinga
manyanyaso ya askari hao.
Baadhi ya madereva wa
mabasi hayo, wamesema wamechoshwa na manyanyaso kutoka kwa askari hao kwa
vitendo vyao vya kuwakamata kiuonevu.
Wamesema sababu kubwa
ya mgomo wao ni rushwa na manyanyaso wanayofanyiwa na baadhi ya askari hao wa
usalama barabarani.
Hata hivyo, akijibu
malalamiko ya madereva hao, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa
Dodoma, Marisone Mwakyoma, amesema sheria zipo wazi kama kuna mtu anaombwa
rushwa na kutoa, wote wana makosa kwa sababu zipo ngazi za kuripoti matukio
hayo.
Afisa Mfawidhi wa
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) mkoa wa Dodoma,
Conrad Shio, amesema baada ya kutokea kwa mgomo huo waliweza kutoa kibali kwa
magari mengine kuweza kubeba abiria wasipate shida ya usafiri.
No comments:
Post a Comment