Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole amesema atahakikisha
chama hicho kinakuwa ni cha wanyonge na kuendelea kuwa kimbilio la wasio na
sauti.
Polepole ametoa kauli
hiyo leo wakati akikabidhiwa rasmi ofisi na Katibu anayemaliza muda wake
Nape Nnauye katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya chama hicho Lumumba jijini Dar
es Salaam.
Polepole alisema kwa
misingi ya chama hicho imejengwa kuwasaidia na kuwa tete wanyongo hivyo katika
muda wake wa uongozi atahakikisha chama kinasimama katima misingi hiyo ya kuanzishwa
kwake.
“Msingi wa chama chetu
ni utetezi wa wanyonge, tutahakikisha kinaendelea kuwa kimbilio la wasio na
sauti,” alisema Polepole.
Aidha, katibu huyo
alisema kuwa katika kutekeleza majukumu yake aliyokabidhiwa leo na mtangulizi
wake, atahakikisha anajikita zaidi katika kazi za itikadi zaidi kuliko uenezi
kwa kuwa itikadi ndiyo inayokibeba chama.
Polepole alitumia muda
huo kumshukuru Nape Nnauye anayemaliza muda wake na kusema kuwa ni kiongozi
imara na kuwa katika muda wake aliweza kuitumikia vyema nafasi yake. Lakini pia
alisema japo anamaliza muda wake, lakini atakuwa akimuhitaji mara kwa mara kwa
ajili ya ushauri na mambo mengine.
Wakati huo huo,
Polepole amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Dkt John Pombe Magufuli na Halmashauri
Kuu ku kumwamini na kumpa majukumu hayo makuwa.
No comments:
Post a Comment