Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametaka apewe taarifa kuhusu
taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) wanaohamasisha au kutangaza
ndoa za jinsia moja nchini ili azifutie usajili mara moja.
Aidha ametaka kutajwa
kwa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo ili wachukuliwe hatua za kisheria kwa
kujihusisha na vitendo hivyo ambavyo vinapigwa vita dunia nzima.
Nchemba aliyasema hayo
jana mjini Kibaha alipokuwa akizungumza na taasisi za Kijeshi za mkoa huo
zikiwemo Uhamiaji, Polisi, Magereza na Zimamoto juu ya kujua changamoto
mbalimbali zinazowakabili.
Alisema kuwa taasisi
hizo hazifai kwani zinafanya kazi ya laana ambayo ni kinyume cha maadili ya
Kitanzania na hazistahili kuendelea kufanya kazi kwa upotoshaji huo.
“Leteni majina ya
taasisi hizo ili tuzifute kwani hazistahili kuendelea kufanya jambo hilo ambalo
ni laana na halipaswi kufumbiwa macho ndani ya jamii,” alisema Nchemba.
Kamanda wa polisi
mkoani Pwani Bonaventura Mushongi alisema kuwa jeshi hilo linakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na upungufu wa vitendea kazi, ikiwa ni
pamoja na magari.
Mushongi alisema kuwa
licha ya kukabiliwa na changamoto hizo wamekuwa wakikabiliana na uhalifu kwenye
mkoa huo ambao umekuwa kimbilio la wahalifu kutoka mikoa jirani ya Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment