Friday 23 February 2018

WANAWAKE WANAOISHI MAENEO YA SHUGHULI ZA UCHIMBAJI KUNUFAIKA KATIKA HILI





Wanawake wapato elfu 70 wanaoishi katika maeneo yenye shughuli za uchimbaji wa dhahabu mkoani Geita wanalengwa kujengewa uwezo wa kiuchumi pamoja na kupatiwa huduma bora za afya.
Hayo yamesemwa na mratibu wa mradi wa The Golden Line,Bi Violet Alphonce unaotekelezwa na chama cha uzazi na malezi bora Tanzania UMAT ambalo ni shirika lisilo la kiserikali kwa kushirikiana na Health Enterpreneur na Solidaridad.

Ufafanuzi huo umetolewa wakati wa kikao cha majadiliano ya utekelezaji mradi huo baina ya shirika hilo na madiwani wa kata tano zinazopatikana katika halmashauri ya mji Geita,halmashauri ya wilaya ya Bukombe na halmashauri ya wilaya Geita.

Mratibu huyo amesema mradi wa The Golden Line unampelekea mwanamke huduma za uzazi salama,uzazi wa mpango,huduma ya magonjwa ya saratani ya shingo ya kizazi na zaidi kumpunguzia mwanamke kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo za uzazi.

Bi Violet aidha katika suala la kumuinua mwanamke kiuchumi amedai kuwa shirika hilo linapigania usawa na kuona mwanaume na mwanamke wote kwa pamoja wananufaika na rasilimali ya dhahabu katika maeneo ya uchimbaji.

Nao baadhi ya madiwani kutoka kata 5 za Katente,Nyaruyeye,Lwamgasa,Nyarugusu na Mgusu ambapo mradi huo unatekelezwa wamedai kuridhishwa na mradi huo na kuahidi kushirikiana kuwapa huduma wananchi wao.

The Golden Line kwa maana ya mstari wa dhahabu ni mradi unaotekelewa kwa miaka 5 na mpaka sasa wanawake zaidi ya elfu 5 wamekwishafikiwa na mradi huo.

No comments:

Post a Comment