Thursday 1 February 2018

BAADHI YA WILAYA MKOANI GEITA ZINAKABILIWA NA UKOSEFU WA MAJENGO YA MAHAKAMA

DSC_1678
Wananchi pamoja na wanasheria wakiwa kwenye maadhimisho ya wiki ya sheria ambayo yamefanyika kwenye viwanja vya mahakama ya Mkoa wa Geita.

DSC_1651
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisalimiana na baadhi ya viongozi wa madhahebu na watumishi wa mahakama wakati alipowasili kwenye viwanja vya maadhimisho ya wiki ya sheria.

DSC_1659
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisalimiana na mwanasheria wa kujitegemea Bernad Otieno wakati alipowasili kwenye viwanja vya maadhimisho ya wiki ya sheria.

DSC_1664
Wanafunzi wa shule ya msingi Kalangalala wakiimba kwenye maadhimisho ya wiki ya mahakama.

DSC_1670
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisaini kitabu cha wageni .

DSC_1671
Baadhi ya mawakili wakiwa meza kuu.

DSC_1697
Mwanasheria wa serikali Mkoani Geita,Emily Kiria akiwakilisha mada ya faida ya matumizi ya mfumo mpya wa TEHAMA utakavyoweza kusaidia utendaji kazi wa mahakama  wakati wa maadhimisho ya wiki ya sheria.

DSC_1706
Wananchi pamoja na watumishi wa mahakama wakimsikiliza wakili wa serikali wakati alipokuwa akiwakilisha mada.

DSC_1738
Kaimu Hakimu Mkazi mfawidhi mahakama ya Mkoa  wa Geita, Ushindi Swalo akijibu baadhi ya mambo ambayo yameelezwa kwenye mada zilizowakilishwa kwenye siku ya maadhimisho ya wiki ya sheria.

DSC_1689
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akimkaribisha Mkuu wa mkoa kwaajili ya kuzungumza na wananchi pamoja na watumishi ambao walikuwa wamejitokeza kwenye maadhimisho ya wiki ya sheria.

DSC_1750
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisisitiza uwajibikaji kwa watumishi wa mahakama pamoja na kutanguliza nidhamu kwa wananchi ambao wanatakiwa kupatiwa majawabu ya kesi zao.

Baadhi ya wilaya za Mbongwe ,Chato,Bukombe na Nyang’hwale Mkoa wa Geita  zinakabiliwa na changamoto  ya ukosefu wa  mahakama za wilaya hali ambayo imekuwa ikisababisha wananchi kwenye maeneo hayo kutembea umbali mrefu kwaajili ya kwenda kusikiliza kesi zao.

Akizungumza kwenye viwanja vya mahakama ya Wilaya ya Geita wakati wa maadhimisho ya wiki ya sheria,Wakili wa serikali Emily Kiria amesema kukosekana kwa mahakama kwenye wilaya hizo ni chanzo kikubwa cha kusababisha ucheleweshaji wa haki kwa wananchi.

Hata hivyo Mkuu wa mkoa wa Geita,mhandisi Robert Luhumbi  ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya sherehe hizo,ameahaidi kuanza ziara ya kuzunguka kwenye wilaya hizo kuhamasisha ujenzi wa majengo ya mahakama kwenye wilaya ambazo zinakabiliwa na uhaba.

Wananchi ambao wapo mjini Geita,Bw Musa Mako na Ally Daniel wamesema mafunzo ya wiki moja ya sheria kwa wananchi hayawezi kusababisha kuelewa hivyo ni vyema kwa mahakama kujenga desturi ya kutoa mafunzo hayo mara kwa mara kutokana na kuwepo kwa tatizo kubwa la uelewa wa sheria na namna ya kuendesha kesi kwa baadhi ya wananchi.

Wiki ya sheria imemalizika leo ikiwa ni mwanzo wa shughuli za mahakama kwa mwaka 2018 huku ikiwa na kauli mbiu isemayo” Matumizi ya Tehama katika utoaji wa haki kwa wakati na kwa kuzingatia maadili”

No comments:

Post a Comment