Sunday 18 February 2018

WAZIRI MWIGULU AMEMUAGIZA IGP SIMON SIRRO KUFANYA UCHUNGUZI KIFO CHA MWANAFUNZI ALIYEPIGWA RISASI

Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Dk. Mwigulu Nchemba  akizungumza na wananchi na baadhi ya viongozi wakati wa shughuli ya uzinduzi wa magereza Wilayani Chato mkoani Geita.

Na Joel Maduka, Chato

Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Dk. Mwigulu Nchemba amemuagiza mkuu wa jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro na timu ya uchunguzi kutoka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina juu ya kupigwa risasi kwa mwanafunzi Akwilina Baftaha ambaye alikuwa ni mwanachuo wa chuo cha usafirishaji (NIT) yaliyotokea wilaya ya kinondoni  jijini Dar es salaam.

Waziri Nchemba ametoa maagizo hayo akiwa mkoani Geita wilaya ya Chato wakati wa uzinduzi wa gereza la wilaya ya Chato.

Waziri Dk. Mwigulu amelitaka jeshi la polisi kuchunguza kwa kina tukio hilo na kujua hatua kwa askari aliyehusika na hilo na kuwaambia wananchi nini kinachoendelea.

"Kama waziri mwenye dhamana nalaani vikali sana tukio la kupoteza maisha ya binti wetu ambaye hakua na hatia, matukio ya namna hii naona yanaanza kujirudia tena kwa kasi matukio ya kupoteza maisha kwa watu wasiokuwa na hatia hasahsa katika maswala yanayohusu siasa ni mambo ambayo hayakubaliki na ninalaani kwa nguvu zote",Alisema Waziri Mwigulu.

Ameongeza kusema kuwa amemuelekeza IGP mala baada ya tukio kutokea wafatilie na wachunguze kubaini wote waliosababisha  tukio la hilo na kuweza kuwafikisha katika mkono sheria ili sheria ichukue mkondo wake.

Dk. Mwigulu amewataka wananchi wote kuepuka vitendo hivi vinavyoweza kusababisha madhara kwa namna moja au nyingine na wanapoona matukio ya namna hii watoe ushilikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili wausika wafikishwe katika vyombo vya usalama.

No comments:

Post a Comment