Tuesday 20 February 2018

RC GEITA AKIRI MGODI WA GGM KUTOKUWA NA TATIZO NA SERIKALI

Mkuu wa mkoa wa Geita,Katikati Mhandisi Robert Luhumbi akiwa ameambatana na  kamati ya ulinzi na usalama akipatiwa maelekezo na moja kati ya wafanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM)wakati alipotembelea mgodi huo kwa lengo la kuona shughuli ambazo zinafanyika mgodini humo.

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akiwa kwenye eneo la uchimbaji la Nyakanga .


Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi  akijaribia moja kati ya magari makubwa ambayo yanafanya kazi za kukusanya mchanga wa dhahabu maarufu kwa jina la dapa.

mtambo ambao   utumiwa kwa shughuli za uchenjuaji ndani ya mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM).
Meneja mahusiano wa mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) Tenga B Tenga akitoa maelezo ya namna ambavyo wamekuwa wakifanya shughuli za uchimbaji ndani ya mgodi wa GGM.
Sehemu ambayo  utumika kusafisha dhahabu kabla ya kutolewa




Mbunge wa Jimbo la Geita mjini ,Cosntatine Kanyasu akielezea  matatizo ambayo yaliyopo kwa wananchi ambayo yalitakiwa yawe yametatuliwa na mgodi wa GGM.

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akizungumza na wadau wa maendeleo pamoja na kamati ya ulinzi na usalama baada ya kutembelea maeneo ya mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM).
Serikali Mkoani Geita imesema kuwa haina tatizo na  Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) na kwamba haiwezi kuendelea kukubali jambo baya ambalo linafanywa na mtu mmoja kuchafua sura ya mgodi mzima kwani  shughuli ambazo zimeendelea kufanywa zimeendelea kuleta manufaa kwa Taifa na mkoa kwa ujumla.

Akizungumza baada ya ziara yake ya kutembelea na kuona namna ambavyo mgodi huo umekuwa ukifanya shughuli za uzalishaji wa dhahabu,Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi alisema  mgodi na serikali  ni kitu kimoja kutokana na kwamba wamekuwa wakilipa fedha kwa Taifa pasipo kuwa na udanganyifu wa aina yoyote.

“Hatuwezi tukakubali jambo lolote lile likafanywa na mtu moja likaonekana uongozi wa mgodi na serikali kwamba hatuna mahusiano mazuri mimi napinga kwa nguvu zote mgodi na serikali tuko kitu kimoja hawa ni wawekezaji wazuri wanalipa fedha zinazotakiwa kwa wakati na kama kuna changamoto chache chache zinaelezeka tukae pamoja tutatue”Alisema Luhumbi.

Kuhusu miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa  na mgodi  huo,Luhumbi alisema kuna makosa mengi ambayo yalifanyika kwa miaka ya nyuma kutokana na miradi ambayo ilikuwa ikipangwa wananchi walikuwa hawafahamu na kwamba kutokana na timu ambayo imewekwa kwa sasa ya mgodi wanaamini   miradi ambayo imepangwa itatekelezwa   kwa   haraka  na  kwa wakati zaidi.

“Makosa mengi yalifanyika katika miradi ya nyumba kosa moja ambalo lilifanyika wewe huwezi kupanga mradi bila ya wananchi kuwa tayari wanafahamu huo mradi na kuna maandalizi mazuri lakini kwa timu ambayo imetengenezwa kwa wakati huu wakurugenzi wote wameshakaa na wamepitisha kwenye vikao  halali vya halmashauri kwa hiyo hili jambo lipo kisheria sana hapa tulipo kuna hatua moja ambayo imebakia ya kuweka sahihi ili miradi ianze kutekelezwa”alisema Luhumbi.

Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi amesikitishwa na kitendo cha mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) kuandika barua kwa viongozi wa makanisa ya Romani na AIC kukataza fedha za maendeleo kupelekwa kwenye miradi suala ambalo sio kweli kutokana na sheria ya mwaka 2017 kubadilishwa ndio chanzo ambacho kinapelekea fedha kujadiliwa na halmashauri husika.

Aidha Meneja mahusiano   huo  Tenga B Tenga  alisema lengo la mgodi ni kuhakikisha wananchi ambao wanauzunguka wananufaika nao kwa nyanja mbali mbali zikiwemo za afya,uchumi pamoja na Elimu.

No comments:

Post a Comment