Friday 23 February 2018

UBOVU WA BARABARA WAKWAMISHA MAENDELEO

Barabara ya mtaa wa Nshinde Kata ya Nyankumbu Wilayani Geita ikiwa imeharibika kutokana na mvua ambazo zinaendelea Kunyesha.

Mwananchi akishindwa kupita na usafiri  kwenye Barabara ambayo imeharibika kwa kiasi kikubwa.

Mwenyekiti wa mtaa wa Shinde Bw,Makoye Mirambo akizungumza juu ya uharibifu huo unavyowaathiri wananchi wake.

Wananchi wa mtaa  wa Nshinde   Wilayani Geita wamelalamikia ubovu wa barabara inayoelekea fadhiri bucha na mwatulole kuwa  kero kubwa kutokana na ubovu ambao umekuwa ukisababisha gari nyingi kukwama na kukosekana kwa baadhi ya huduma za usafiri.

Akizungumza na mtandao huu Bi Fatuma mwita  amesema tatizo hilo ni la muda mrefu  na bado halijapatiwa ufumbuzi jambo ambalo linapelekea usumbufu katika harakati zao za kutafuta maendeleo na kwamba wamekuwa wakipata shida pindi hususani mvua zinaponyesha.

Aidha ameongeza  kuwa wamekuwa wanapata usumbufu mkubwa kutokana na kuwepo mashimo katika barabara hiyo na kupelekea baadhi ya madereva kukataa kupita na wengine hali ambayo imeendelea kusababisha kuendelea kuharibika kwa barabara.



“Inafika wakati watoto wanashindwa kwenda shule kutokana na ubovu huu wa barabara jamani yani huku sisi tumekuwa kama tupo kisiwani ambapo akuna huduma nzuri  tunaomba serikali isikie kilio chetu itusaidie” Alisema Fatuma.

Naye  Bw,Emmanuel John alisema ubovu wa barabara hiyo umechangia  baadhi ya madereva wa  piki piki kushindwa kufika hata pindi wanapokuwa na wagonjwa hivyo kujikuta wakipata shida kubwa zaidi kutokana na ubovu huo.

Hata hivyo Diwani wa kata hiyo,Michael Kapaya alikili  kuwepo kwa ubovu wa barabara hizo na kwamba kwa sasa bajeti za utengenezaji unafanywa na TARURA na wamekwisha kuziingiza kwenye bajeti hivyo anatarajia muda wowote zitaanza kujengwa.

Kaimu meneja wa Tarura halmashauri ya mji Bw ILDEPHONCE ZIRIRA   amesema ujenzi wa barabara unaenda kwa hatua kwa hatua na kwamba wamekwisha pereka bajeti ya mwaka 2018 /19  hivyo anaamini mwaka huu zitajengwa kwenye maeneo ambayo yanachangamoto kubwa ya uharibifu.

No comments:

Post a Comment