Monday 5 February 2018

MAADHIMISHO YA MIAKA 41 YA CCM YALETA TUMAINI JIPYA KWA WAGONJWA WILAYANI GEITA

DSC_1682
Mjumbe wa Baraza kuu Taifa Mkoani Geita, ,Bw  Charles Kazungu  Akitoa msaada kwa Bi, Teddy Saidi wakati wa zoezi la kutoa misaada katika kuadhimisha miaka 41 ya chama cha mapinduzi Wilayani Geita.

DSC_1684
Baadhi ya wajumbe wa chama cha mapinduzi wakiwa wameambatana na Mjumbe wa Baraza kuu Taifa Mkoani Geita, ,Bw  Charles Kazungu wakitoa msaada kwa mtoto Zuberi Juma.

DSC_1671
Wajumbe wa chama cha mapinduzi (CCM)wakiongozana na katibu wa  chama hicho Julius Peter na Diwani wa Kata ya Kalangalala Sospeter Mahushi wakati wakielekea kutoa  misaada kwa wagonjwa ambao wapo kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita.

DSC_1693
Mjumbe wa Baraza kuu Taifa Mkoani Geita, ,Bw  Charles Kazungu akitoa msaada kwa Bw,Fredy Magunga.


DSC_1702
Katibu wa chama cha mapinduzi(CCM)Julius Peter akitoa pole kwa mgojwa ambaye alikuwa kwenye wodi ya wakinamama Hospitali ya Rufaa ya Mkoani Geita.

Consolata Evarist.Geita


Chama Cha Mapinduzi(CCM) Wilayani  Geita  kimeadhimisha miaka Arobaini na moja (41) tangu kuzaliwa  kwa kuwatembea wagonjwa na kutoa misaada mbali mbali kwenye hospatali ya Rufaa ya mkoani humo.

Zoezi hilo limeendeshwa na uongozi wa chama na baadhi ya wanachama  wakiambatana na  Mjumbe wa Baraza kuu Taifa ambaye alikuwa ni mgeni Rasmi ,Bw  Charles Kazungu  alisema maamuzi ya kutembelea hospitali ya mkoa ni kutaka kujua namna ambavyo ilani ya chama hicho inavyotekelezwa kwenye  sekta ya afya.

Aidha ametoa wito kwa watumishi wa Sekta hiyo kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia taratibu na sheria ambazo zimewekwa na nchi.

Natoa wito kwa watumishi ambao wanatabiaya kutokutoa huduma vizuri kwa wagonjwa kuachana na tabia hiyo  rai yangu waweze kutimiza adhima na kazi zao utawala wa chama cha mapinduzi hususani awamu ya tano unataka wafanye kazi kwa mujibu na sheria nasi vinginevyo”, alisema Kazungu

Kazungu alisema katika kuhakikisha serikali inajali wananchi wake imeonelea  ni vyema maadhimisho kwa ngazi ya wilaya wakayafanyia  hospalini na kutoa msaada wa kuwasaidia watu ambao wanauwitaji maalumu kama wagonjwa.

Pia amewataka  wananchi kufika katika vituo vya afya kwani vimeboreshwa kwa kiasi kikubwa na vina hudumia kwa umakini mkubwa hivyo wasipendelee kukaa na magonjwa nyumbani wanaweza kusababisha vifo na matatizo makubwa ambayo yange weza kuzuilika.

kwa upande wake katibu wa umoja wa wazazi Wilaya ya Geita,Happynes James  ameiasa jamii pindi inapopata matatizo ya kiafya ni vyema wakafika kwenye vituo vya afya ili kujua ni matatizo gani ambayo yanawasumbua na kuachana na dhana ya kukimbilia wa waganga wa kienyeji

Baadhi ya wagonjwa akiwemo Teddy Mathayo na Juma Mabeyo wameishukuru serikali pamoja na chama cha mapinduzi (CCM) kwa msaada ambao wameutoa kwa moyo walio uonesha wakuonesha kujali na kuwafariji kwa kiasi kile walicho balikiwa  na kwamba wamefarijika sana kwa tukio hilo .

No comments:

Post a Comment