Friday 16 February 2018

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATOA TAMKO KUHUSU KIDATO CHA TANO


Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa kila kijiji kinakuwa na shule ya msingi yenye madarasa ya awali na kila tarafa iwe na shule ya kidato cha tano na cha sita.
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo jana  Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza katika ziara yake ya siku saba mkoani Mwanza ambapo amewasisitiza walimu wasijiingize katika masuala ya michango bali wajikite na taaluma.

Waziri Mkuu Majaliwa katika siku yake ya kwanza mkoani humo akiongozana na  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,  alizindua madarasa manne ya kidato cha tano katika shule ya sekondari ya Nyehunge wilayani  sengerema huko na kutoa maagizo hayo.

No comments:

Post a Comment