Thursday 15 February 2018

MGODI WA ACACIA BULYANHULU WAENDELEA KUSHIRIKIANA NA JAMII KWENYE MIRADI YA MAENDELEO

Mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala ,Simon Berege  akikata utepe kuzindua rasmi jengo la maktaba katika shule ya sekondari Bulyanhulu. Kaulia ni kaimu  Meneja mkuu wa mgodi wa  Bulyanhulu Elias Kasitila.Na katikati  ni Mwakilishi wa shirika la Read International ,Esther Kalwinzi .
Wanafunzi wa Shule ya sekondari Bulyanhulu wakionesha vipaji mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuruka sarakasi.

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Bulyanhulu wakifuatilia burudani mbali mbali zinazoendelea wakati wa hafra ya uzinduzi wa Maktaba.

Walimu wa shule ya sekondari ya Bulyanhulu wakicheza mziki wakati wa hafra fupi ya uzinduzi wa Maktaba.

Muonekano wa jengo la maktaba katika shule ya sekondari Bulyanhulu lililoboreshwa na mgodi wa Bulyanhulu  kwa kushirikiana na Read International .

Afisa elimu wa sekondari halmashauri ya msalala,Bw Christopha Machele akiwatambulisha baadhi ya wajumbe ambao wanatokea kwenye halmashauri hiyo.

Mwakilishi wa shirika la Read International ,Esther Kalwinzi akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa jengo la maktaba katika shule ya sekondari Bulyanhulu .

Mwakilishi wa shirika la Read International ,Esther Kalwinzi akionesha sehemu ya kuangalia orodha ya aina za vitabu vilivyopo katika maktaba kwa mkurugenzi wa  halmashauri ya msalala , Simon Berege .

Mkurugenzi wa  halmashauri ya msalala , Simon Berege akiangalia moja kati ya vitabu ambavyo vimo kwenye maktaba hiyo.

Muonekano wa maktaba ya shule ya sekondari Bulyanhulu

Kaimu Meneja mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu Elias Kasitila  akielezea namna walivyoshirikiana na shirika la Read International katika kufanikisha ukarabati wa jengo hilo la maktaba.
Mkurugenzi wa  halmashauri ya msalala , Simon Berege akizungumza na wananchi baada ya ufunguzi wa maktaba ya shule ya sekondary ya  Bulyanhulu.


Mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu umezindua na kukabidhi  maktaba iliyogharimu shilingi milioni 22.6  kwenye shule ya sekondari Bulyanhulu  iliyopo katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani  wa Shinyanga kwa lengo la kusaidia wanafunzi na walimu  katika kuboresha ubora wa elimu inayotolewa.


Maktaba hiyo imezinduliwa  na Mkurugenzi  mtendaji wa halmashauri ya Msalala Bw , Simon Berege  na kuhudhuriwa  na  kaimu Meneja  mkuu wa Mgodi wa  Bulyanhulu,Elias Kasitila.

Akizungumza wakati uzinduzi huo, Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi  Bulyanhulu,Elias Kasitila alisema wakati wakitafakari namna ya kuinua taaluma ya wanafunzi waliona ni vyema wakaimarisha usomaji wa wanafunzi kwa kuwekeza kwenye  maktaba ambayo  itasaidia kuboresha upatikanaji wa elimu kwa wanafunzi kutoka kwa  jamii inayouzunguka mgodi huo.

Alisema  kupitia mpango wa Acacia wa maendeleo ya jamii wameamua kushirikiana na shirika la kimataifa la Read International kuboresha jengo moja la shule hiyo na kuliwekea samani kwa ajili ya matumizi ya maktaba ambayo itawasaidia wanafunzi na walimu kwa kiasi kikubwa.

“Misaada inayotolewa na Acacia katika sekta ya elimu ni sehemu ya sera ya wajibikaji kwa jamii ya kampuni inayojikita katika kuhakikisha jamii inakuwa endelevu kupitia sekta ya elimu na sera hiyo inachangia moja kwa moja maono ya taifa hadi kufikia mwaka 2025 na malengo ya nchi ya kuleta maendeleo endelevu kwa kuhakikisha jamii inapata elimu iliyo bora”,alisema Kasitila.

Mwakilishi wa shirika la Read International linalojihusisha na masuala ya elimu,Esther Kalwinzi alisema pesa ambazo zimetolewa na mgodi huo ni shilingi milioni 22.6 kwa ajili kukarabati darasa kuwa maktaba.

Kwa upande wake,mgeni rasmi katika hafla hiyo,Mkurugenzi wa Halmashauri ya msalala , Simon Berege umeushukuru   mgodi huo  pamoja na shirika la Read International kwa kufadhili maktaba hiyo ya kisasa kwenye shule hiyo na kwamba itasaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kujisomea na kujenga uwezo mkubwa kwenye masomo yao.

Kikubwa zaidi ninacho wasisitiza wanafunzi kuzingatia masomo  na pia wazazi tambueni elimu ndiyo urithi pekee wa kudumu na wenye kubadilisha maisha ya mtoto kutoka hali ya chini ya  umasikini kuja juu zaidi  kimaisha”Alisisitiza Berege.

Hata hivyo mmoja kati ya wanafunzi wa shule hiyo  Mussa Rajabu alisema  kuzinduliwa kwa maktaba hiyo kutaleta  chachu ya kupenda kujisomea zaidi na kwamba itawasaidia kufanya vizuri kwenye masomo yao.

No comments:

Post a Comment