Friday 16 February 2018

WANANCHI WATAKIWA KUSHIRIKI KWENYE MIRADI YA MAENDELEO MJINI GEITA

Mchanga wa kujengea vyumba vya madarasa ukimwagwa kwenye uwanja wa shule ya Sekondari ya Mwatulole huku baadhi ya viongozi wa kata pamoja na wadau wa elimu  wakishuhudia mchanga huo wakati ulipokuwa ukimwagwa.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinaly akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa vifaa vya ujenzi kutoka kwa mdau wa Elimu kwenye shule ya Sekondary ya Mwatulole.

Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondary ya Mwatulole,Bi Roselyine Mdariki akishukuru kuwenza kupatiwa msaada huo kwenye shule hiyo ambao utasaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa. 

Mzee Devid Ng’ombeyapi akielezea namna ambavyo aliguswa na kuamua kuchangia kwenye sekta ya Elimu. 

Baadhi ya vyumba vya  madarasa kwenye shule ya Sekondary Mwatulole.

Mzee Devid Ng’ombeyapi akibidhi seruji kwa Diwani wa kata ya Buhala hala( kushoto) Musa Kabese Pamoja na kwa mkuu wa shule ya Sekondary ya Mwatulole Bi,Roselyine Mdariki. 

Wakazi wa Halmashauri ya mji wa Geita wameombwa kuendelea kuunga Mkono jitihada za kutoa michango mbalimbali itakayosaidia kuboresha miundombinu ya Elimu.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Mhandisi Modest Apolinary wakati akipokea mifuko 10 ya seruji na tripu mbili za mchanga kwenye shule ya sekondari ya Mwatulole kutoka kwa mwananchi aliyejitolea kwa lengo la kusaidia ujenzi wa mabweni shuleni hapo.

Alisema suala la kutoa michango alijakataliwa jambo ambalo lilizuiliwa ni walimu kuendelea kujihusisha na kupokea michango na wengine walikuwa wakiwarudisha wanafunzi sababu tu ya kukosa michango jambo ambalo sio sahihi  na kwamba kwa mtu ambaye anaguswa ni vyema wakawasiliana na ofisi ya mkurugenzi mtendaji.

Aidha kwa upande wake Mkuu wa shule ya sekondari mwatulole  Bi,Roselyine Mdariki mbali na kushukuru kwa msaada huo ameelezea changamoto ambayo wanaipata kwa sasa shuleni hapo ni upungufu wa madarasa  kwani kwa mwaka huu wamepokea wanafunzi wengi zaidi wa kidato cha kwanza ukilinganisha na miaka iliyopita.

“Shule yetu imekuwa na changamoto ya vyumba vya madarasa kutokana na ongezeko la wanafunzi kwa mwaka huu na kutokana na ongezeko hilo mkurugenzi wetu wa halmashauri ameamua kutuunga mkono kwa kutupatia mifuko ya seruji mia moja tunaamini itasaidia kwa kiasi kikubwa ujenzi wa vyumba vya madarasa shuleni hapa”Alisema Mdariki.

Hata hivyo diwani wa kata ya Buhala hala,Musa Kabese ,alisema changamoto kwenye kata yake ni  ni upungufu mkubwa wa madarasa  ambapo vinaitaji vyumba  kumi na moja  hili kukidhi mahitaji kwa shule mbili za  sekondari mwatulole pamoja na kalangalala .



Kwa upande wake mwananchi ambaye ametoa msaada huo,Devid Ng’ombeyapi alisema kilichopelekea kutoa ni kutokana na kuguswa na namna ambavyo wanafunzi wamekuwa wakipata shida  ya upungufu wa vyumba vya madarasa shuleni hapo.

No comments:

Post a Comment