Wednesday 31 January 2018

RC GEITA MH. ROBERT LUHUMBI AWATAHADHALISHA WATENDAJI AMBAO WANATAFUNA PESA ZA MIRADI

DSC_1561
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akishiriki na wananchi wa kijiji cha Bukuru kata ya Kafita wilaya ya Nyang’hwale ujenzi wa kituo cha afya cha kijiji hapo.

DSC_1535
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akikagua madarasa kwenye shule ya sekondari ya Nyachiluluma Wilayani  Nyang’hwale

DSC_1570
Baadhi ya wakina mama wa Kijiji cha Bukuru wakishiriki shughuli za ujenzi wa kituo cha afya.

DSC_1587
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akizungumza na wanakijiji wa kijiji cha Bukuru wakati wa ziara ya kuhamasisha maendeleo.

DSC_1596
Zahanati ya Mwamakiliga ambayo ameizindua Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi.

DSC_1632
Mkuu wa Mkoa wa Geita mhandisi Robert Luhumbi akikagua baadhi ya vyumba vya zahanati ya Mwamakiliga.

DSC_1641
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akikata utepe wakati wa uzinduzi wa zahanati ya Mwamakiliga.


Serikali Mkoani Geita imewataka wananchi ambao wameendelea kujitolea kwenye shughuli za maendeleo hususani ujenzi wa vituo vya afya, zahanati na shule kuendelea na juhudi hizo na kwamba Serikali ipo pamoja  nao kuunga jitihada hizo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Geita mhandisi Robert Luhumbi wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Bukuru Kata ya Kafita Wilayani Nyang’hwale kwenye kampeni aliyoianzisha ya kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na zahanati na kituo cha afya ifikapo Desemba mwaka huu.

Alisema serikali inatambua juhudi zinazoendelea kufanywa na baadhi ya wananchi wenye mapenzi mema na kwamba serikali hipo nao bega kwa bega kuhakikisha inawasaidia kutimiza malengo ambayo wamejiwekea kwenye maeneo yao.

Akisoma taarifa ya uanzishwaji wa zahanati ya Kijiji hicho kwa niaba ya mtendaji Mwl Timotheo Daniel Njogomi alisema hatua hiyo imekuja baada ya kukosekana kwa huduma za afya na kuwalazimu wananchi kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hizo hali ambayo imeendelea kupelekea waakina mama wajawazito kujifungulia njiani.

Bw John Isack ambaye ni diwani wa kata hiyo alisema amekuwa akishirikiana na viongozi na wananchi wengine katika kujenga zahanati kwenye vijiji vya kata yake ambavyo bado vinachangamoto kubwa zaidi.

Sanjari na hayo Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Bw Hamim Gweyama amewataka watumishi kutumia vema fedha za miradi zinazopelekwa kwenye maeneo yao.

No comments:

Post a Comment