Monday 19 September 2016

WAZIRI NAPE AHIDI KUTOA MILLIONI KWA KILA GOLI LITAKALOFUNGWA NA SERENGETI BOYS KATIKA MECHI YA MARUDIANO NCHINI CONGO BRAZAVILLE.



Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwasili katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kushuhudia mechi kati ya Serengeti Boys na Congo Brazaville ambapo Serengetri iliibuka na ushindi wa Goli 3 kwa 2.





Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akishanglia pamoja na mashabiki katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza katika mechi kati ya Serengeti Boys na Congo Brazaville ambapo Serengetri iliibuka na ushindi wa Goli 3 kwa 2.



Mshambuliaji wa Serengeti Boys Yohana Oscar Nkomolo akishangilia mara baada ya kufunga bao la pili dhidi ya Congo Brazaville katika Uwanja  wa Taifa Jijini Dar es Slaam Serengeti ilishinda kwa jumla ya goli 3 kwa 2.







Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wachezaji wa Serengeti Boys na waandishi wa habari  Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa mechi yao dhidi ya Congo-Brazaville iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016 Serengeti ilishinda kwa jumla ya goli 3 kwa 2.



Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwapongeza  wachezaji wa Serengeti Boys Jijini Dar es Salaam mara  baada ya  kumalizika kwa mechi yao dhidi ya Congo-Brazaville iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016 Serengeti ilishinda kwa jumla ya goli 3 kwa 2.


Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana ya Serengeti Boys wakiwashukuru mashabiki mara baada ya katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa mechi kati yao na Congo Brazaville ambapo Serengeti Boys iliibuka na ushindi wa goli 3 kwa 2.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ameahidi kutoa  kiasi cha shilingi Millioni moja kwa kila goli litakalofungwa na Serengeti Boys katika mechi ya marudiano nchini Congo Brazaville.

Ametoa ahadi hiyo wakati akiongea na kuwapongeza wachezaji hao mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 kati ya Serengeti Boys ya Tanzania na Congo Brazaville uliofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

“Kwa niaba ya Watanzania wote nawapongeza kwa mchezo mzuri mliouonesha na kuibuka na ushindi lakini bado mnatakiwa kujituma kama mlivyofanya katika mechi hii na naahidi kutekeleza ile ahadi yangu ya laki tano kwa kila goli na nitatoa tena kwenu Millioni moja kwa kila goli mtakalofunga Congo Brazaville.”Alisema Mhe. Waziri Nape.

Kwa upande wa Kocha wa Timu hiyo Bw. Bakari  Shime ameshukuru Waziri na Watanzania kwa ujumla kwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mechi hiyo na watahakikisha wanapata ushindi katika mechi ya marudiano kwani wameshayaona mapungufu yaliyojitokeza na watayafanyia kazi wachezaji watakuwa tayari kuivaa tena Congo Brazavile.

Aidha Nahodha wa Timu  hiyo Bw. Issa Abdi Makame mbali na kuishukuru Serikali kwa motisha inayotoa ameahidi kujituma zaidi kwa kushirikiana na wenzake na  kufuata maagizo kutoka   Bechi la ufundi  ili kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo wa marudiano.

“Tunashukuru sana kwa motisha mnayotupa na sisi hatutawaangusha tutajituma kadri ya uwezo wetu tupate ushindi tukiwa ugenini ili tuweze kufuzu” Aliongeza Nahodha Makame.

Timu ya Taifa ya Tanzania ya  vijana chini ya  umri wa Miaka kumi na saba (Serengeti Boys) inayowania tiketi ya kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) kwa vijana yatakayofanyika nchini Madagascar mwaka 2017 inatakiwa kupata ushindi ili kujihakikishia kufuzu kwa fainali hizo.


No comments:

Post a Comment