Monday 26 September 2016

MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI YAMEZINDULIWA RASMI LEO MKOANI GEITA



naibu waziri wa mambo ya ndani Mhandisi Hamad Masauni azindua wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani, Kitaifa Mjini Geita leo


Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiyaangalia maandamano ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani.


Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Mohamed Mpinga akizungumza katika Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani.

Washiriki wa maonyesho (waendesha bodaboda) wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani mjini Geita leo.

Maadhimisho  ya  Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani yamezinduliwa Rasmi leo Mkoani Geita katika viwanja vya Kalangalala  na Naibu Waziri wa mambo ndani Mh.Ahamed Masauni, huku ajali za waendesha piki piki maarufu  boda boda zikiendelea kushika kasi kubwa  zaidi nchini.
Akitoa taarifa ya jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamanda  wa kikosi cha usalama Barabarani Nchini Mohamed Mpinga amesema  kuwa Baraza la taifa la usalama barabarani nchini limekuwa na mikakati mbali mbali  ya kukabiliana na ajali ambazo zimekuwa zikijitokeza hususani ni zile ambazo zinachangaiwa  na uzembe barabarani.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa  Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano   Mhandisi  Edwin Ngonyani ambaye ni mwenyekiti wa baraza la usalama barabarani nchini, amefafanua kuwa pamoja na jitihada ambazo zinafanywa na Serikali bado kuna tatizo kubwa la Madereva na wapanda pikipiki  kutokujali Sheria  na kanuni za usalama barabarani.
Aidha mgeni rasimi katika  maadhimisho hayo Mh.Ahamed masauni  amemtaka kila mtumiaji wa barabara kupambana  kwa nguvu na mali katika kutokomeza ajali  za barabarani na kwamba wajibu huu sio wa serikali   tu bali wananchi nao wanahusika huku akitaja idadi ya ajali zilizotokea kwa mwaka huu.

Mkuu wa mkoa wa geita Meja Jenerali Mstafu ezekiel Kyunga ametoa Shukrani kwa Baraza  la  Usalama Barabarani  kufanyia maadhimisho ya wiki ya nedna kwa usalama barabarani mkoani geita akiamini kuwa ni moja kati ya njia ya kutangaza Mkoa wa Geita.

No comments:

Post a Comment