Wednesday 7 September 2016

TASWIRA MBALIMBLI MBUNGENI LEO MJINI DODOMA





Baadhi ya Wabunge wakiingia katika ukumbi wa bunge kuhudhuria kikao cha 2 cha bunge la kumi na moja  la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania



Mbunge wa Jimbo la Urambo Mhe.Margaret Sitta akimueleza Jambo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo Mjini Dodoma.


Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akijibu swali wakati wa kikao cha 2 cha bunge la Jmahuri ya Muungano wa Tanzania ambapo alitoa wito kwa waajiri nchini kuwasilisha nyaraka za wastaafu kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii miezi mitatu hadi sita kabla ya kustaafu kwa wateja wao ili kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba Leo Bungeni Mjini Dodoma.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kintinku  mkoni Singida wakifuatili vikao vya Bunge leo Mjini Dodoma


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akijibu swali wakati wa kikao cha 2 cha bunge la Jmahuri ya Muungano wa Tanzania ambapo alisema serikali haina mgogoro wowote wa mafuta baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar leo Mjini Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Wazee na Wenye Ulemavu  Mhe. Jenista Mhagama (MB) akimueleza jambo Mwansheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju leo Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Andrew Chenge akiongoza kikao cha Bunge leo Mjini Dodoma
Mbunge wa Jimbo la Kaliua Mhe. Magdalena Sakaya akiuliza swali wakati wa Kikao cha Pili cha Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment