Wednesday 21 September 2016

RAIS WA BOTSWANA AMTAKA ROBERT MUGABE AJIUZULU



Rais wa Botswana kushoto Ian Khama na mwenzake wa Zimbabwe Robert Mugabe
Rais wa Botswana Ian Khama amemtaka Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kujiuzulu mara moja kulingana na chombo cha habari cha Reuters.
Ameambia Reuters kuwa taifa la Zimbabwe linahitaji uongozi mpya ili kukabiliana na changaomoto za kisiasa na za kiuchumi zinazokabili taifa hilo.
“Ni wazi kwamba umri wake na hali ambayo Zimbabwe ipo kwa sasa hana uwezo wa kutoa uongozi ambao unaweza kulinusuru taifa hilo,”.
Bwana Mugabe ameliongoza taifa hilo tangu uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1980.
Bwana Khama amemlaumu kiongozi huyo kwa tatizo linalokabili uchumi wa eneo hilo.
Amesema mgogoro uliopo Zimbabwe umewafanya raia wengi kulitoroka taifa hilo,huku wengine wakielekea Botswana ambayo inawahifadhi zaidi raia 100,000 wa Zimbabwe.

Khama anasema kuwa ataondoka afisini mwaka 2018 baada ya kuhudumu kwa mihula miwili ,huku akiwashtumu viongozi wanaotaka kusalia madarakani kwa mda mrefu.

No comments:

Post a Comment