Wednesday 21 September 2016

WATU WENGINE KADHAA WAUAWA KATIKA MAANDAMANO NCHINI CONGO DRC



Waandamanaji nchini Congo DRC

Watu wengine kadhaa wameuawa katika siku ya pili ya machafuko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jana, huku makao makuu ya vyama vitatu vya upinzani yakichomwa moto.
Hayo yamejiri katika wimbi jipya la makabiliano kati ya polisi na wapinzani wa Rais wa nchi hiyo Joseph Kabila 
Machafuko yalizuka upya baada ya Jumatatu ya umwagaji damu ambapo makundi ya upinzani yamesema zaidi ya watu 50 walikufa katika maandamano ya kudai Rais Kabila ajiuzulu.

Katibu wa chama kikuu cha upinzani cha Union for Democracy and Social Progress (UDPS), Felix Tshisekedi amelilaumu kundi la makomando la utawala kwa kuyachoma makao makuu ya upinzani.

Maiti mbili zilizoungua zimeonekana katika afisi za chama hicho.

Waandishi wa habari wa shirika la habari la Ufaransa, AFP wamesema watu wengine wawili wamechomwa wakiwa hai na mwingine mmoja kujeruhiwa.

No comments:

Post a Comment