Saturday 3 September 2016

SHIRIKA LA MAENDELEO YA VIWANDA NCHINI(NDC) LATAKIWA KUONGEZA VIWANDA ZAIDI



Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwigaje akiongea na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Maendeleo  (NDC) wakati akiizindua leo Jijini Dar es Salaam, ambapo ameitaka bodi hiyo kushika miradi mikubwa ya uwekezaji na kuhakikisha inairudisha katika hali yake ili kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati kupitia uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda


Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wakimsikiliza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwigaje, wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo, Leo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Viwanda ,Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema Shirika la  Taifa Maendeleo ya Viwanda (NDC) ndio injini ya inayoendesha sekta ya viwanda na hivyo inatakiwa kuhakikisha ndani ya miaka minne inakuwa  viwanda hata vitatu katika kuweza kufikia uchumi wa kati.

Mwijage ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa Bodi mpya ya Wakurugenzi ya shirika hilo,ambapo ameitaka bodi kufanya kazi ili kuhakikisha inashikilia viwanda vikubwa ambayo vitafanya taifa kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.

Amesema kuwa kazi ya bodi hiyo kwa kuaznia ni kuangalia miradi na viwanda ambavyo kwa sasa havifanyi vizuri ikiwamo mradi wa Liganga na Mchuchuma, kiwanda cha matairi cha general tyre kilichopo Arusha na vingine ili na dhumuni ni kuhakikisha vinaanza kuzalisha.

Mwijage amesema kuwa  kutokana bodi hiyo kuwa na watu wa kila sekta muhimu hivyo wanahitaji kukutana mara kwa mara hata bila kulipwa posho ili mambo yeande na kuleta tija kwa taifa.

Amesema kuwa miradi mikubwa ikikamilika nchi itakuwa imepiga hatua kimaendeleo na kuweza kufikia uchumi wa kati  wa viwanda vyenye manufaa kwa wananchi.

Nae Mwenyekiti wa bodi wa NDC,  Dk, Samwel Nyantahe amesema kuwa watafanya kazi kwa karibu na Wizara ikiwa ni pamoja na kutembelea miradi yote na kuweza kuanza kufanya kazi kwa nguvu.

Amesema Rais Dk. John Magufuli amemuamini hivyo watatimiza wajibu kwa kushirikiana na bodi hiyo katika sekta ya viwanda.

No comments:

Post a Comment