Wednesday 21 September 2016

M-PAWA KUTOKA VODACOM YAZIDI KUWATAJIRISHA WATANZANIA MSHINDI WA PILI APATIKANA



 Meneja masoko Huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania ,Noel Mazoya (katikati) akiongea na mmoja wa mshindi wa droo ya promosheni ya Jiongeza na M-Pawa wakati wa hafla ya kuchezesha droo ya pili ya wiki iliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo mkazi wa Arusha Isaack Pilemon alijishindia kitita cha shilingi Milioni 20. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Meneja wa Huduma za M-Pawa wa Benki ya CBA Eric Luyangi na Msimamizi wa bodi ya michezo ya Kubahatisha nchini Bakari Maggid
Jumla ya shilingi milioni 300 zimetengwa kwa ajili ya promosheni hiyo na mshindi mmoja wa droo kubwa atajishindia kitita cha shilingi milioni 100. Washindi wa wiki watazawadiwa shilingi milioni 20 na washindi wa siku watazawadiwa shilingi milioni moja.

Promosheni hiyo ambayo ilianza mwanzoni mwa mwezi wa 9 itadumu kwa kipindi cha wiki sita na itafikia kilele mwishoni mwa Mwezi Oktoba, 2016.

No comments:

Post a Comment