Monday 25 July 2016

YANGA WAKAMUA SANA GHANA, KAZI WANAYO MEDEAMA KESHO

Yanga imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa shule ya Bohar mjini hapa kujiandaa na mchezo wa Jumanne dhidi ya wenyeji, Medeama ya Ghana.
Yanga iliyowasili Ghana usiku wa jana kutoka Dar es Salaam imepania kushinda Jumanne ili kufufua matumaini ya kwenda Nusu Fainali.

Mchezo Hao utachezeshwa naRedouane Jiyed atakayepuliza filimbi akisaidiwa na Mohamed Lahmidi na Hicham Ait Abbou watakaoshika vibendera.

Yanga SC iliondoka bila beki Mtogo mwenye asili ya Ivory Coast, Vincent Bossou abaye ameeachwa Dar es Salaam.

Bossou ambaye anatumikia adhabu ya kadi mbili za njano ni kati ya wachezaji watatu waliobaki Dar es Salaam, wengine wakiwa ni viungo Geoffrey Mwashiuya na Deus Kaseke ambao ni majeruhi.


Lakini kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm amesema pengo la Bossou litazibwa na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye yuko fiti.

“Tuna viungo wa kutosha, sifurahii kuwakosa Kaseke na Mwashiuya, lakini kwa kuwa hawapo kwa sababau ambazo zipo nje uya uwezo wetu, wengine watacheza badala yao,”aliema Pluijm juzi usiku kabla ya safariya Ghana.

Yanga watakuwa wageni wa Medeama Jumanne ya Julai 26, mwaka huu Uwanja wa Sekondi Sports au Essipong mjini Sekondi-Takoradi, Ghana katika mchezo huo wa kwanza wa marudiano mzunguko wa pili Kombe la Shirikisho, na siku inayofuata vinara wa kundi hilo, TP Mazembe wataikaribisha Mouloudia Olympique Bejaia mjini Lubumbashi.

Timu hizo zitarudiana kiasi cha wiki baada ya kutoa sare katika mechi zao za kwanza, Yanhga 1-1 na Medema ana MO Bejaia 0-0 na Mazembe.

Mazembe inaongoza Kundi A kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na MO Bejaia pointi tano, Medeama pointi mbili, wakati Yanga yenye pointi moja inashika mkia.  

No comments:

Post a Comment