Monday 11 July 2016

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI NCHINI AZINDUA MPANGO WA NISHATI ENDELEVU KWA WOTE



Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo akionyesha jalida maalum wakati wa uzinduzi wa mpango wa Nishati endelevu kwa wote(SE4ALL) wenye lengo la kuhakikisha upatikanaji wa nishati yauhakika kufikia mwaka 2030.Kushoto kwake ni Mratibu mkazi washirika  la umoja wa Mataifa na mwakilishi washirika la Maendeleo la Kimataifa Bw.Alvaro Rodrigez(UNDP) na Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa benki ya Maendeleo ya Afrika Bi.Tonia Kandiero.
Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo amezindua mpango wa Nishati endelevu kwa wote (SE4ALL) wenye lengo la kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika kufikia mwaka 2030, wakati akiindua mpango huo amesema kuwa uwekezaji wa umeme Vijijini awamu ya tatu utagharimu zaidi ya Trilioni moja.


Mpango huu umelenga kufanikiwa mwaka 2030, lakini kwa sisi Tanzania kabla ya mwaka huo tutakuwa na umeme kwa kila mtanzania na Programu hii italifanya taifa letu lijulikane duniani kwani tuna dhamira ya kumfanya kila mtu apate umeme”
utasaidia suala la ajira na kutokomeza umaskini, kwaiyo kama nchi tuko katika ngazi za juu za huu mradi katika kuufanikisha tukishirikiana na wadau mbalimbali

Aidha amesema kuwa Programu hii ya Umoja wa Mataifa itasaidia sana katika kuongeza vyanzo vya kuzalisha umeme kwani inafanana sana na ile ya kwetu ya Taifa ambapo tutazalisha umeme mwingi kutokana na gesi, makaa ya mawe, umeme wa maporomoko ya maji, umeme wa Jua, joto ardhi na mabaki ya mimea.

Amesema mashirika mengi yamesaidia katika kufanikisha upatikanaji wa umeme vijijini ikiwemo benki ya Dunia ambayo imetoa dola milioni 200, Umoja wa Ulaya umetoa euro 180, Nchi za Nordic zimetoa dola milioni 300 pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika nayo imetoa fedha katika kuwekeza kwenye umeme vijijini pia.

No comments:

Post a Comment