Friday 8 July 2016

APIGWA MPAKA KUPOTEZA MAISHA KWA WIZI WA KUKU WILAYANI SENGEREMA


Mwanaume mmoja ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 mpaka 40 jina halijafahamika, ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na kupigwa hadi kupoteza maisha  na wananchi wenye hasira kali  baada yakumkamata akifanya kitendo cha wizi wa kuku 7
Mtu huyo aliyepigwa na marungu, alifanya kitendo hicho kipindi cha sikukuu ya Eid.
Taarifa ya tukio hilo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi, na kusema tukio hilo limetokea baada ya mtu aliyeibiwa kuku hao kuomba msaada kwa wananchi na wananchi kumkamata mwizi huyo na kuanza kumpiga na silaha hizo mpaka kumsababishia mauti.

Kamanda Msangi amesema jeshi la polisi mkoani humo linawashikilia watu watatu kwaajili ya mahojiano ya tukio hilo na kuwataka watanzania kuacha kufanya vitendo vya kiharifu kwa kisingizio cha kukosa ajira za kuwaingizia kipato cha kila siku, kwani vitendo hivyo vya kiharifu vinagharimu maisha yao na kuwasababishia kifo.


Amewaasa watanzania kuacha kujichukulia sheria mkononi na watumie vyombo vya usalama katika kupambana na wahalifu.

No comments:

Post a Comment