Wednesday 20 July 2016

SERIKALI KUENDELEA KUPAMBANA NA KUPINGA UTUMIKISHWAJI WA WATOTO NCHINI.



Mwakilishi wa Shirika la Watoto Duniani(UNICEF) Bi.Cecilia Baldeh akieleza jambo wakati  wa uzinduzi wa matokeo ya utafiti wa utumikishwaji wa watoto wa mwaka 2014 Tanzania Bara uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango leo jijini Dar es Salaam.



Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt Albina Chuwa akitoa maelezo mafupi kuhusu ripoti ya matokeo utafiti wa utumikishwaji wa watoto wa mwaka 2014 Tanzania Bara uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango leo jijini Dar es Salaam.



Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Dk. Abdallah Possi akizungumza kabla hajazindua  matokeo ya utafiti wa utumikishwaji wa watoto wa mwaka 2014 Tanzania Bara uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango leo jijini Dar es Salaam.



Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Dk. Abdallah Possi akionyesha ripoti ya  matokeo ya utafiti wa utumikishwaji wa watoto wa mwaka 2014 Tanzania Bara mara baada ya kuizindua leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Kazi Dunia Tanzania Bw,Jealous Chirove.




Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Dk. Abdallah Possi akimkabidhi ripoti ya  matokeo ya utafiti wa utumikishwaji wa watoto wa mwaka 2014 Tanzania Bara mwakilishi wa Shirika la kazi Duniani,Geneva Bw.Azfar Khan leo jijini Dar es Salaam

Serikali imesema kuwa itaendelea kupambana na kupinga utumikishwaji wa watoto nchini ili tuwe na Taifa imara.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge, Kazi, Vijana, Ajira  na Walemavu  Dk.Abdallah Possi alipokuwa akizindua ripoti ya matokeo ya utafiti wa utumikishwaji wa watoto wa mwaka 2014 Tanzania Bara Jijini Dar es Salaam ambayo imeonyesha kuwa utumikishwjai wa watoto umepungua kutoka asilimia 30.1 mwaka 2006 mpaka asilimia 28.8 mwaka 2014.

Dk Possi alisema kuwa Jitihada mbalimbali zinaendela kufanywa na serikali ya awamu ya Tano ikiwemo utoaji wa Elimu bure ili kuhamasisha mahudhurio ya watoto shuleni na kupunguza uwezo wa watoto kujihusisha na ajira za utotoni.

Aidha Naibu Waziri uyo alisema kuwa utafiti huo umebaini kuwa takribani watoto milioni 5 wanajihusisha na shughuli za kiuchumi, miongoni mwao wasichana ni asilimia  52.5 na wavulana ni asilimia 47.5 ambayo kwa ujumla katika watoto wa tatu mmoja anajihusisha katika shughuli za kiuchumi uku sekta ya kilimo,misitu na uvuvi ndo zimebeba asilimia 92.1 ya watoto wote wanaojihusisha na shughuli za kiuchumi.

Aidha ripoti hiyo imeonyesha kuwa watoto wanaotumikishwa vijijini ni wengi kuliko mijini na hivyo maendeleo ya kiuchumi ni muhimu katika kuhakikisha ajira kwa watoto zinatokomezwa na kwa hili serikali inaendelea kuhakikisha kuwa elimu na maendeleo vijijini yanapatikana ili kuondoa tatizo hilo.

Kwa upande wa elimu ripoti inaonyesha kuwa watoto wanaoishi mijini hutumia muda mwingi kujisomea tofauti na walioko vijijini ambapo watoto wanaoishi Dar es Salaam hutumia muda mrefu zaidi katika kujisomea ambapo ni sawa na asilimia 19.9 ikifuatiwa na maeneo mengine ya mjini ambao hutumia asilimia 17.8 ya muda wao kwa siku kwa kujisomea na watoto wa vijijini walitumia asilimia 14.4 kwa ajili ya shughuli za kujisomea.

Naye Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt Albina Chuwa amesema kuwa ripoti hii itasaidia katika kutengeneza sera nzuri za maendeleo na kudai kuwa kila mtu ana jukumu la kuhakikisha watoto wanalindwa na kuacha kutumikishwa katika shughuli za kiuchumi na pia taasisi yake imejiandaa vyema katika kutumia mfumo mpya na wa kisasa unaoitwa E-popular register ili kupata takwimu ambazo zinaendana na wakati.


Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Watoto Duniani(UNICEF) Bi.Cecilia Baldeh amesema kuwa asilimia 29 ya watoto duniani wanatumikishwa katika shughuli za kiuchumi na hivyo kukosa haki yao ya msingi ya kusoma na kuiomba serikali kufuatilia kwa karibu mazingira ya kazi yanayohusisha watoto na kushauri kuwekwa kwa mfumo wa kijamii ambao utasaidia kufatilia na  kuwalinda watoto katika Nyanja zote.

No comments:

Post a Comment