Friday 8 July 2016

VIONGOZI WA DINI MKOANI GEITA WAPONGEZA SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA MGODI WA DHAHABU WA GEITA(GGM)


Umoja  wa madhehebu ya kikristo na  kiislamu Interface Mkoani Geita, imeupongeza mgodi  wa  dhahabu   wa GGM, kwa  juhudi  ambazo umekuwa   ukizifanya  za kuhakikisha kwamba wananchi    wananufaika kutokana  na  uwepo  wa mgodi huo.

 Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea kalakana ya ufundi   iliyopo eneo la magogo  kata ya Bomba mbili  walipokuwa  wamekwenda kutembelea  eneo hilo kwa lengo la kuona shughuli  zinazofanywa na kalakana hiyo.

 Mratibu wa Interface  mchungaji John Marko Ndaruka amesema  kuwa wameendelea kufaidika na GGM kutokana na huduma ambazo kwa sasa zinaonekana kwani hapo awali  huduma hizo zilikuwa hazifahamiki hivyo wananchi   wengi  walikuwa hawaoni  faida ya uwepo wa mgodi   huo.

Kwa upande wake, shekhe Alhad  Yusufu  Kabaju ambae ni mwenyekiti mwenza  wa taasisi  hiyo  ameongeza kuwa kumekuwepo na maneno kwa jamii kuwaona kwamba hakuna jambo lolote linalofanywa na GGM, kwani sababu kuu ni kutokana na viongozi wa serikali kutokuelezwa kazi ambazo zinafanywa na mgodi   katika  kuleta maendeleo.



Meneja Mahusiano wa Mgodi wa dhahabu Manase Ndoloma ameeleza kuwa  thamani ya miradi inaweza kufikisha Dola milioni moja endapo kila kitu kitakuwa kimekamilika  katika kalakana hiyo.

No comments:

Post a Comment