Tuesday 26 July 2016

WATANZANIA WAASWA KUWA WAMOJA KWENYE UJENZI WA NCHI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiongea leo na wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania na kuwaasa watanzania kudumisha amani ambayo ilipatikana baada ya Mashujaa wetu kuipigania na hata kujitoa uhai wao kwa ajili ya Taifa.



Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili  Mheshimiwa Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiongea leo na wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania na kuwataka watanzania kumuunga mkono Mhe. Rais Dkt. Magufuli katika harakati za kuijenga Tanzania mpya.



Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa  Dkt.Ali Mohamedi Shein akiongea leo na wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania na kusisitiza kuhusu umuhimu wa watanzania kuenzi amani iliyoasisiwa na wazee wetu na kuacha kushiriki katika vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani.



Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Samweli Malechela akiongea leo na wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania na kumshukuru kwa kusimamia na kutekeleza ahadi zilizowahi kutolewa na hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwemo kuhamishia serikali Mkoani Dodoma.



Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa akiongea leo na wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania na kumuahidi Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa atahakikisha anasimamia utekelezaji wa maagizo ya kuitaka Serikali ihamie mjini Dodoma.


Mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa baada ya kuwekwa kwa silaha za asili za mashujaa na maua




Baadhi ya wananchi wakifuatilia shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania katika viwanja vya Mashujaa vilivyopo mjini Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika viwanja vya Mashujaa vilivyopo mjini Dodoma wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiweka silaha za asili kwenye Mnara wa Mashujaa leo Mkoani Dodoma wakati wa shughuli ya maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania

No comments:

Post a Comment