Monday 25 July 2016

SERENGETI BOYS KUELEKEA KAMBINI MADAGASCAR KESHO

Shirikisho la Soka nchini TFF Alfredy Lucas amesema, kikosi hicho kitaondoka kikiwa na wachezaji 19 viongozi wanne, Kiongozi mkuu Ayubu Nyenzi, kocha mkuu Bakary Shime, mshauri wa ufundi kwa soka la vijana Kim Poulsen,kit manager, na daktari wa timu.
Lucas amesema, kocha msaidizi Sebastian Nkoma ambaye anashiriki kozi ya daraja A ya CAF na kocha wa makipa wa Serengeti Boys Mwarami Mohamed Sultan anayeshiriki kozi ya makipa ya kiwango cha daraja B hawatakuwa katika msafara huo hivyo nafasi zao zitachukuliwa na Mlinda Mlango Juma Kaseja ambaye atashikilia nafasi zote.
Wachezaji wanaoondoka ni Makipa: Kelvin Deoglas, Ramadhan Kabwili na Samweli Edward.
Mabeki: Kibwana Shomary, Nickson Kibabage, Israel Mwenda, Dickson Job, Ally Msengi na Issa Makamba.
Viungo: Kelvin Nashon, Ally Ng'anzi, Assad Juma, Cyprian Mtesigwa na Shaaban Adda.
Washambuliaji: Enrick Nkosi, Ibrahim Ally, Mohamed Rashid, Yohana Mkomola na Muhsin Makame.

No comments:

Post a Comment