Tuesday 5 July 2016

WAKUU WAPYA WA WILAYA ZOTE MKOANI GEITA WATAKIWA KUHAKIKISHA SUALA LA ULINZI NA USALAMA


Mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga amewaagiza wakuu wapya  wa wilaya zote mkoani Geita kuhakikisha wanadhibiti  suala la watu ambao wamekuwa wakiingia  mkoani hapa  kutoka nchi jirani kinyume na taratibu za sheria ya  nchi kwa kushirikiana na kamati za ulinzi na usalama zilizopo katika wilaya wanazoziongoza.

Kyunga ameyasema hayo jana  katika Hafla fupi ya kuwaapisha wakuu wa wilaya tano zilizopo mkoani hapa iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi za mkuu wa mkoa
Amesema kuwa  suala la ulinzi na usalama ni muhimu sana katika jitihada za kuleta maendeleo ya wananchi hivyo ni vyema wakawa makini kwa kudhibiti mipaka ya wilaya zao ikiwa ni pamoja na kuwadhibiti  wageni wanaoingea nchini kwa njia za zisizo halali.

aidha Kyunga ameendelea kuwaagiza wakuu wa wilaya kuakikisha wanasimamia taratibu mbali mbali za kuhakikisha wanatokomeza ujambazi ambao umekuwa ukijitokeza mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kushirikiana na mabalozi wa nyumba kumi ambao wamekuwa wakihakikisha wanalinda maeneo wanayoyaongoza katika mitaa yao.


Hata hivyo miongoni mwa wakuu wa wilaya hao kutoka katika wilaya ya Geita na Mbongwe  Herman Kapufi na  Matha m Mkapusi wamesema kuwa ili kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa ni vyema wananchi wawaunge mkono ili kuhakikisha uhalifu unatokomezwa.

No comments:

Post a Comment