Wednesday 20 July 2016

AJALI YASABABISHA VIFO VYA WATU WAWILI MKOANI GEITA


Ajali  imetokea  jana majira ya saa tano za Asubuhi   katika eneo la Rukilini, Wilayani na Mkoani Geita na kusababisha watu 15 kujeruhiwa  huku mtu mmoja  akipoteza maisha  wakati akipatiwa   matibabu

Ajali hiyo imehusisha gari aina ya Toyota Hiace yenye nambari za usajili T 859 BFC lililokuwa likitokea mjini Geita kuelekea katika kijiji  cha  Senga.

Wakielezea  namna na jinsi tukio hilo lilivyokuwa baadhi ya majeruhia  Bw.Edward  Shaban  na Kassim  Nyombo wamesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na walipo jaribu kumshauri dereva kupunguza mwendo aliwaambia kuwa anatakiwa kuwahi.

Storm  habari ,ilifanikiwa kufika katika hospitali teule ya Mkoa na kuzungumza na Dokta Mahenga Makoye ambae yupo katika kitengo cha dharula na  kusema kuwa majira ya saa saba mchana ndipo walipofika majeruhi na wengine walikuwa katika hali mbaya zaidi.


Aidha  mkuu wa kitengo cha usalama barabarani Mkoani hapa Alfred Hussein  amesema kuwa hadi sasa wanaendelea kuchunguza chanzo cha ajali hiyo na kwamba dereva ametoweka baada ya kusababisha ajali hiyo lakini bado wanaendelea na uchunguzi zaidi ili kubaini nini chanzo cha Ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment