Thursday 28 July 2016

JOSEPH SENGA ALIYEPIGA PICHA ZA TUKIO LA MAUAJI YA MWANDISHI WA HABARI DAUD MWANGOSI AFARIKI DUNIA




Simanzi yatanda siku moja baada ya mahakama kuu kanda ya Iringa kumhukumu kifungo cha  miaka kumi na mitano Askari  aliyemuua Daudi Mwangosi. Tasnia ya habari yapata pigo,mpiga picha wa gazeti la Tanzania aliyepiga picha za tukio la mauaji ya Daudi ya Mwangosi,JOSEPH SENGA amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Bila Joseph Senga, Shujaa aliyehatarisha maisha yake,akasimama bila woga,akapiga picha na kuzitunza,akafichua mauaji,asingekuwa Senga,nadhani leo kusingekuwa na kesi na mwisho hukumu dhidi ya aliyemuua Mwangosi.

Senga,Senga,Senga,Senga,umekwenda,Mungu aliamua akuweke hai mpaka hukumu itoke na mwisho  amekuchukua,Senga umekwenda wadogo zako katika tasnia tukiwa na hamu ya kujifunza kutoka kwako.

Senga,Senga,kamsalimie Daudi Mwangosi,mwabie aliyemuua nae kahukumiwa jela miaka 15,kamwambie mazingira ya waandishi wa habari bado magumu.

Nenda Senga, picha zako zinabaki kuwa rejea ya mafunzo ya uandishi wa habari katika mazingira hatarishi.


No comments:

Post a Comment