Thursday 26 January 2017

WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA KWA KUKOSA HEWA NDANI YA KISIMA



Watu wawili wamefariki Dunia papo hapo katika mamlaka ya mji mdogo  wa Katoro Wilayani na Mkoani Geita baada ya kukosa hewa katika shimo la kisima  ambalo waliingia kwa lengo la kupasua mwamba  uliokuwa  umetanda  katika kisima hicho.
Tukio hilo limetokea  jana Januari 26 mwaka huu majira ya saa tano asubuhi  katika nyumba ya kulala wageni  ijulikanayo  kwa jina la Mlimani B Guest House iliyopo mtaa  wa kilima hewa  miliki ya Bw. Cosmas Mayala ambapo  watu  hao waliingia katika shimo hilo  kupitia katika mlango mdogo  wa kisima hicho kisha kuwasha moto wa mkaa ndani ya shimo hilo linalo kadiliwa kuwa na urefu wa futi 30  ndipo  mmoja kati ya marehemu hao aliingia  katika shimo hilo kwa lengo la kuangalia moto walio uwasha kama umewaka vizuri  alikaa kwa muda mrefu bila majibu ndipo  mwenzie alipo chukua jukumu la kwenda kumuangalia ndani ya shimo hilo lakini na yeye pia hakufanikiwa kutoka.

Baadhi ya wakazi katika eneo hilo kwa kushilikiana na jeshi la zima moto  na uokoaji kutoka mjini geita walitumia takribani saa tatu kuitoa miili ya marehemu katika shimo hilo.


Aidha  mwenyekiti  wa mtaa huo Bw.Isaack Lufungulo  amewataja  walio fariki dunia kuwa   ni Lucas Bukelebe anaekadiliwa kuwa na umri wa miaka 42 mkazi wa katoro mzaliwa wa Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza pamoja na Silvester John mwenye umri wa miaka 36 mkazi wa Katoro mzaliwa wa Ngara mkoani Kagera .

No comments:

Post a Comment