Monday 23 January 2017

UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI NKOME WAMALIZIKA KWA USALAMA


Baadhi ya wananchi wakisikiliza kwa makini maelekezo ya kupiga kura kutoka kwa msimamizi 


Askari polisi wakiimarisha ulinzi katika kituo cha kupigia kura
Kata ya Nkome wilaya na Mkoa wa Geita, imefanya uchaguzi mdogo wa udiwani huku hali ya ulinzi na usalama ikitawala katika kipindi chote cha upigaji wa kura.

Msimamizi mkuu wa uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Ali Kidwaka  ameelezea kuwa zoezi hilo limefanyika katika hali ya utulivu na kwamba jumla ya vituo thelathini na nane (38) vimehusika kufanya uchaguzi.

Kuhusu  ulinzi na usalama Kidwaka amesema kuwa hali ilikuwa tulivu hakuna fujo wala usumbufu wowote ambao umeweza kujitokeza lakini nje ya vituo kuna masuala yalijitokeza ya uvunjifu wa amani na utulivu.

Baadhi ya wananchi wa kata hiyo Hussein Omary ameeleza kuwa uchaguzi ambao umefanyika  katika hali nzuri kwani hayupo ambaye ameshindwa kupiga kura vituo vyote vilikuwa wazi na kwamba kila mtu alikuwa ana uhuru wa kumchagua yule ambaye anaona yupo sahihi kumwongoza.


Naye Bi.Flora Mussa amesema kuwa wao kama wazee wanaishukuru serikali kwani hakuna buguza ambayo wamekutana nayo na kwamba wamekuwa wakipewa nafasi ya upendeleo na kuthaminiwa katika chumba cha uchaguzi.

No comments:

Post a Comment