Saturday 21 January 2017

WASANII MKOANI GEITA WATOA WITO KWA SERIKALI



Mwenyekiti wa chama cha wasanii Mkoani Geita,Rose Michael (ROSE BONANZA)akisoma risala wakati wa ufunguzi wa mashindano ya wasanii wa maigizo na nyimbo mbele ya mgeni rasmi kwenye ukumbi wa halmashauri ya mji wa Geita.
Chama cha wasanii Mkoani Geita,kimeiomba serikali Mkoani humo kuendelea kutoa ushirikiano katika Nyanja hiyo muhimu ikiwa ni pamoja na  kusapoti kazi  ambazo zimekuwa zikifanywa  na wasanii.

Kauli hiyo imesemwa na mwenyekiti wa chama hicho Mkoani Humo Rose Michael wakati wa ufunguzi wa mashindano ya kuwasaka wasanii wenye vipaji vya kuimba, kuigiza na kuchekesha yaliyokuwa yanafanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Mji wa Geita.

Bi.Rose alisema kuwa Tasnia ya sanaa bado inachangamoto nyingi ikiwa ni pamojan na kushindwa kutambulika na kushikwa mkono  kwenye serikali kutokana na kwamba baadhi  viongozi wa kiserikali wanaona swala la wasanii limekaa kiunu jambo ambalo si kweli kwani  kazi ya sanaa ni sawa na shughuli zingine katika jamii.

“Sisi wasanii bado tunachangamoto kubwa sana katika serikali ingawa kwa sasa kuna wizara inayotutambua lakini bado kuna ugumu mwingi tu tukiangali kwenye serikali kuna viongozi ambao wanaona kuwa hatuna mchango wowote lakini sio kweli sisi tunauwezo wa kufikisha ujumbe kwa jamii na ikatuelewa zaidi kuliko vile ambavyo serikali imeendelea kutuchukulia”alisema Rose.

Kwa upande wake mwenyekiti wa waigizaji Mkoa wa Mwanza,Ramadhani  Masululi,amesema kuwa jambo ambalo limekuwa likisababisha sanaa au wasanii kuonekana ni wahuni ni kutokana na baadhi ya wasanii kuonekana kutokujieshimu na wengine kuingia kwenye sanaa bila ya kuwa na maono au mtazamo chanya katika sanaa.

“Sanaa sio uhuni kwanini wanasema uhuni waigizaji  wengine wameingia ni mamluki unakuta mwingine anaingia kwenye sanaa ni mlevi mvuta bangi na mwingine ni Malaya na hii ya wezekana kwasababu nikutokana na vigezo kutokuwa vigumu lakini sisi kama chama  cha wasanii hatuwezi kukubaliana na swala hili tutaakikisha wale wenyetabia za ajabu wanatupisha ili tuwe na wasanii ambao wananidhamu”alisema Ramadhani


Akimwakilisha Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Geita ambaye ndiye alikuwa mgeni rasimi kwenye uzinduzi huo,afisa maendeleo ya jamii wa halmashauri hiyo,Maiga Majagi,amewaasa wasanii kutumia umoja wao  kuleta mabadiliko kwa wanageita kwa kufanya kazi na kukitumia chama chao kwa kuwa tetea zaidi na kupata taarifa  mbali mbali za soko la kazi zao na pia amewataka  kupanga mikakati ya kushirikiana  na wadau wote  na kwamba jambo likiongelewa na wote linakuwa na nguvu kuliko kuzungumziwa na mtu mmoja.

No comments:

Post a Comment