Wednesday 25 January 2017

TMAA YAJIDHATITI KUKUSANYA MAPATO SEKTA YA MADINI



Kaimu Mkuu wa Kitengo  Cha  Habari toka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Mhandisi Yisambi Shiwa akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu mafanikio ya wakala huo katika kipindi cha Julai-Desemba 2016 ikiwemo kufanikiwa kukusanya Bilioni 79.26 zilizolipwa Serikalini na Kampuni za Madini kama kodi ya mapato. Kushoto ni Meneja Utafiti  na Mipango wa Wakala huo Bw. Julius Moshi na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Uzalishaji na Biashara ya Madini Migodi Mikubwa, ya Kati na Midogo Mhandisi Baraka Manyama.



Meneja  Utafiti na Mipango wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Bw. Julius Moshi akitoa ufafanuzi kuhusu hatua zinazochukuliwa na wakala huo katika kuhakikisha kuwa Serikali inakusanya mapato yote yanayotokana na Madini.



Meneja wa uthamini wa Madini Bw.George Kaseza akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu mikakati ya wakala huo kusimamia vyema sekta ya madini ili iweze kulinufaisha Taifa. Kulia ni Meneja Utafiti na MipangowaWakala waUkaguzi waMadini Tanzania (TMAA) Bw. Julius Moshi.


Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) leo Jijini Dar es salaam.


Kaimu  Mkurugenzi Uzalishaji na Biashara ya madini migodi mikubwa,ya kati na midogo Mhandisi Baraka Manyama akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kupatikana kwa malipo  ya mrabaha kutokana na shughuli za uchenjuaji wa marudio kwa kutumia teknolojia ya VAT LEACHING. Kulia ni Meneja wa uthamini wa Madini Bw.George Kaseza na kushoto ni Meneja Utafiti  na Mipango Bw. Julius Moshi.


 Kaimu Mkurugenzi wa ukaguzi wa hesabu za Kodi  na fedha za Migodi Bw. Venance Bahati akieleza kwa waandishi wa Habari kuhusu mikakati ya wakala huo kukagua migodi yote na kuhakikisha kuwa Kodi zote zinalipwa Serikalini kwa kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya madini , kulia ni Meneja wa uthamini wa Madini Bw.George Kaseza na  kushoto ni Meneja Utafiti na Mipango Bw. Julius Moshi.

No comments:

Post a Comment