Tuesday 10 January 2017

WANANCHI WA KATORO MKOANI GEITA WALALAMIKA JUU YA WAENDESHA PIKIPIKI



Wananchi  wa mamlaka ya mji mdogo wa katoro wilayani na mkoani Geita wamelalamikia kitendo cha waendesha pikipiki pamoja na wafanyabiashara ndogondogo katika mtaa wa Lutozo  kuegesha pikipiki  zao kando ya barabara jambo ambalo lina hatarisha usalama wa watembea kwa miguu kutokana  na kuwepo kwa msongamano  uliokithiri.
Wakizungumza  mapema hii leo kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa eneo hilo wameiomba Serikali kupanua barabara hiyo ili iweze kupunguza msongamano pia kuondoa adha  waipatayo watembea kwa miguu pindi watakapo kuvuka  barabara hiyo kuelekea upande wa pili.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa huo Bw. Jonathan Mchele amesema kuwa atashirikiana na jeshi la polisi kikamilifu  kuhakikisha wanaliweka eneo hilo salama kwa watembea kwa miguu hasa wanafunzi.


Hata hivyo Diwani wa kata hiyo ya katoro Bw. Benedect Kigongo amewataka wakazi wa eneo hilo kuwa wavumilivu kwani suala hilo atalifanyia kazi.

No comments:

Post a Comment