Thursday 26 January 2017

WATU 14 WAMEFUKIWA NA UDONGO KWENYE MGODI




Watu  kumi na nne (14) mmoja akiwa  ni  Raia  wa China  wamefukiwa na udongo usiku  wa kuamkia leo majira  ya saa saba usiku wakiwa wanaendelea na majukumu  yao  ya uchimbaji kwenye  kampuni  ya  RZ  iliyopo kijiji cha Nyarugusu wilayani na mkoa wa Geita.
Juhudi  za  ukoaji zinaendelea  katika eneo hilo  huku  sababu  za kuporomoka  udongo  ni kutokana  na  mgodi kuchimbwa  zamani   na wajerumani   hivyo kupelekea baadhi ya maeneo hayo  kuwa na nyufa na vyuma kushindwa kushikilia udongo  wa  juu hali ambayo imepelekea kuzidiwa na kuporomoka.

Kamati  ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Geita imefika katika  Mgodi  wa  RZ kuangalia  zoezi  la ukoaji katika mgodi na kamisha msaidizi wa madini kanda ya ziwa  victoria Mhandisi Yahaya Samamba ameelezea hali ilivyo na jitihada za uokoaji zinavyoendelea .

Kamanda  wa  Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Geita, Elisha  Mugisha amesema  kuwa  eneo la chini  ambalo limefukiwa na udongo   ndio  ambalo kwa sasa  wanaendelea kulitanua  ili  sehemu hiyo iwe  kubwa  watu  waweze kupita.

 Mwanasheria na msemajiwa Kampuni ya uchimbaji Dhahabu ya RZ  Fransis  Kiganga anaelezea sababu za Mgodi   huo kuporomokewa  na udongo.

Baadhi ya wafanyakazi  wa Kampuni hiyo Charles Julius  na Robert Stanley ambao  ni wachimbaji wa kampuni hiyo wanaelezea hali ilivyokuwa na namna ilivyotokea.


Aidha mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali mstaafu ezekiel kyunga amewataka wanaosimamia   zoezi la uokoaji   kuongeza   nguvu ya uokozi.

No comments:

Post a Comment