Thursday 26 January 2017

MA RC, DC WAAGIZWA KUHAKIKISHA WANACHUKUA HATUA DHIDI YA TATIZO LA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene akizindua kitabu cha Mwongozo wa Taifa wa Utekelezaji wa Sera za Huduma kwa watoto waliokatika mazingira hatarishi kwa Serikali za Mitaa leo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Misaada na Maendeleo la Marekani (USAID)  nchini Tanzania Tim Donnay, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI Dkt. Zainab Chaula na Msaidizi wa Waziri wa Nchi TAMISEMI
Wakuu wa mikoa na wilaya nchini wametakiwa kuhakikisha wanatafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na kuacha  kufanya kazi kwa   mazoea.

Agizo hilo limetolewa na waziri wa nchi ofisi ya Rais, tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza mkutano wa pili wa majadiliano baina ya tamisemi na shirika la maendeleo la Marekani (USAID) pamoja na uzinduzi wa muongozo wa taifa wa utekelezaji wa Sera za huduma kwa watoto walio katika mazingira hatarishi leo jijini Dar es salaam.

Aidha Simbachawene ameongeza kuwa serikali za mitaa zinao wajibu wa kuwahudumia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwani ndiyo watekelezaji wa sera mbalimbali ikiwemo sera ya watoto, viongozi wa serikali za mitaa wasiishie  tu kuwaondoa watoto mitaani bila ya kutafuta   kiini  na suluhisho  la    tatizo   hilo.

Sanjari na hilo Simbachawene amempongeza Katibu mkuu wa Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto kwa kazi nzuri  ya utafiti ambayo imebaini kuwa rasilimali nyingi zinazotengwa kwa ajili ya kuhudumia afya ya mama na mtoto haziwafikii walengwa ambapo amesema kuwa hiyo  ni changamoto kubwa.

Ameongeza kuwa Serikali ya awamu  ya tano chini ya Rais Magufuli inasisitiza uwazi na uwajibikaji hivyo panapotokea kuwa uzembe unatokana na utendaji mbovu miongoni mwao si vyema wakafumbia macho badala yake inapaswa waseme ukweli ili wahusika wajirekebishe na kuchukuliwa hatua stahiki.

No comments:

Post a Comment