Tuesday 17 January 2017

PICHA:KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YATEMBELEA BANDARI



Wajumbe wa Kamati ya Bajeti wakiendelea na Kikao.



Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa Ghasia (Mb) akizungumza wakati Kamati hiyo  ilipotembelea Bandari ya Dar es Salaam.


Naibu Waziri wa UjenziUchukuzi na Mawasiliano MheInjinia Edwin Ngonyani (Mb) (wa kwanza kulia) akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Bajeti wakati Kamati hiyo ilipotembelea Bandari ya Dar es Salaam mapema leo. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Hawa Ghasia(Mb). Kamati za Kudumu za  Bunge zimeanza shughuli zake hii leo ambapo katika wiki hii takribani Kamati za Kisekta 12 zitakuwa zikifanya ziara za kukagua miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini  kabla ya kurejea Mjini Dodoma kwa ajili kuendelea na vikao vyake.



Kaimu Meneja wa Bandari wa Dar es Salaam Bw. Nelson Mlali akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakati wa ziara hiyo.


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa Ghasia (Mb) akimueleza  jambo Kaimu Meneja wa Bandari wa Dar es Salaam Bw. Nelson Mlali wakati wa ziara hiyo.



No comments:

Post a Comment