Monday 30 January 2017

WAHANGA 15 WALIOFUKIWA NA MGODI WA RZ WARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALINI LEO



Mchungaji wa Kanisa  FPCT Geita Mathias Gundula  ,Akimshukuru Mungu juu ya yale ambayo ameyateda kwa vijana ambao wameokolewa kutoka mgodini.



Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga akiwasalimia wachimbaji ambao walikuwa wamefukiwa na kifusi kwenye Mgodi wa RZ,katika Hosptali ya Rufaa ya Geita.

Wahanga  15  wakiwemo watanzania 14 na Raia mmoja wa kichina  walionusurika na  kifo baada ya kuokolewa kutoka chini ya ardhi kwenye  mgodi wa dhahabu wa RZ Union ulioko  kijiji cha Mawe-meru  kata ya Nyarugusu mkoani Geita baada ya kukaa siku 3 bila chakula wala huduma wameruhusiwa kutoka hospital ya mkoa wa geita walikopelekwa kupata matibabu.
Akiwaaga baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali mkuu wa mkoa  Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amewaomba kurudi na kuendelea kujituma katika shughuli ambazo wanafanya  ili kuendelea na ujenzi wa taifa.

Hata hivyo mkuu wa Wilaya ya geita Herman Kapufi,amesema kuwa wamekubaliana na mgodi huo wafanyakazi wote katika mgodi huo kupatiwa mkataba ambao utawasaidia wafanyakazi na pia amewaomba kuwa na mahusiano mazuri baina ya wafanyakazi na waajiri ambo ni raia wa china na pia amewasisitiza kumrudia mungu kwani amewanusuru na kifo.

Aidha kwa upande wake mwanasheria wa mgodi huo Francis Kiganga pamoja na kuyashukuru mashirika ambayo yamejitolea kufanya  shughuli  za uokoaji  pia amemwakikishia mkuu  wa wilaya kuongeza mkataba wa kazi badala ya miezi mitatu  atawapatia wa mwaka mzima.

Akiwaruhusu wahanga hao, mganga mfawidhi wa hospitali ya Mkoa wa Geita Dkt. Brian Mawalla amesema wamefikia uamuzi wa kuwaruhusu baada ya kujiridhisha na maendeleo mazuri ya afya zao.

Wahanga hao wameokolewa January 29 mwaka huu kwa msaada kutoka makampuni ya Busolwa Mining, Nyarugusu , Geita Gold Mine(GGM) , na ACACIA Mining wamefanikiwa kuwaokoa watu hao waliofukiwa na udongo wa kifusi cha mgodi huo januari 26 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment