Uingereza imetoa
mchango wa Shilingi Bilioni 6 kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuchangia
ujenzi wa miundombinu ya shule zilizopata madhara kufuatia tetemeko la ardhi
lililotokea katika Mkoa wa Kagera tarehe 10 Septemba, 2016.
KUHABARISHA NA KUFAHAMISHA KUHUSU HABARI NA MAMBO YANAYOENDELEA KATIKA JAMII YA GEITA, KANDA YA ZIWA, TAIFA NA DUNIANI. TUTUMIE HABARI AU WASILIANA NASI KUPITIA info@stormfm.co.tz au +255 685 883 870
Thursday, 29 September 2016
Wednesday, 28 September 2016
SPIKA MSTAAFU SAMWELI SITTA APELEKWA UJERUMANI KUTIBIWA
Hali ya Afya ya Spika
mstaafu, Samuel Sitta si nzuri,baada ya Serikali kumpeleka nchini Ujerumani kwa
matibabu zaidi.
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA KOREA YA KUSINI
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amekutana na wawekezaji wa kampuni
tisa za nchini Korea Kusini na kumuahidi kushirikiana na Serikali ya
Tanzania kuwekeza katika sekta ya kilimo, viwanda, maji, miundombinu, elimu,
afya na michezo.
Tuesday, 27 September 2016
BARAZA KUU LA UONGOZI CUF LAMFUTA UANACHAMA PROFESA LIPUMBA
Baraza Kuu la Uongozi
la Chama cha Wananchi (CUF) Taifa lililokutana Zanzibar leo limemfukuza
uanachama Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Prof. Ibrahim Lipumba.
BABA AJINYONGA BAADA YA KUMPIGA BINTI YAKE HADI KUPOTEZA MAISHA MKOANI GEITA

Mtoto mmoja anayejulikana kwa jina la Martha Charles Mwenye umri wa miaka 15
ameuwawa kwa kupigwa na fimbo na Baba yake mzazi kisha baba yake
aliyefahamika kwa jina la Charles Mlima kujinyonga baada ya tukio hilo
lilitokea katika kata na kijiji cha kaseme wilayani na Mkoani Geita.
Akizungumza na Stormfm ndugu wa familia hiyo John
Lufunguro amesema kuwa marehemu ambae ni mtoto wa Baba huyo
alikumbwa na mauti hayo baada ya kupigwa na baba yake kwa kile
kilichodaiwa kuwa amekutwa katika hali ya kimapenzi, hali ambayo
haikumpendeza baba yake kutokana na kuwa na umri mdogo kujiingiza katika
mahusiano ya kimapenzi.
NDEGE YA PILI YA BOMBARDIER Q-400 YAWASILI JIJINI DAR ES SALAAM LEO, RAIS MAGUFULI KUZIZINDUA NDEGE HIZO KESHO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kesho anatarajiwa kuzindua ndege mbili mpya
aina ya Bombardier Q 400 zilizonunuliwa na Serikali hivi karibuni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leornard Chamuriho amesema maandalizi yote kwa ajili ya uzinduzi wa ndege hizo yamekamilika na uzinduzi huo utafanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Kesho kuanzia saa mbili asubuhi.
“Tunawaomba wanahabari na wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo ili waone utekelezaji wa ahadi wa Serikali katika mkakati wa kuhuisha usafiri wa Anga hapa nchini”, amesema Dkt. Chamuriho.
Ndege hizo aina ya Bombardier Q 400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja zimetengenezwa nchini Canada na zitahudumia soko la ndani ndani na nchi za jirani zitakapoanza kazi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leornard Chamuriho amesema maandalizi yote kwa ajili ya uzinduzi wa ndege hizo yamekamilika na uzinduzi huo utafanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Kesho kuanzia saa mbili asubuhi.
“Tunawaomba wanahabari na wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo ili waone utekelezaji wa ahadi wa Serikali katika mkakati wa kuhuisha usafiri wa Anga hapa nchini”, amesema Dkt. Chamuriho.
Ndege hizo aina ya Bombardier Q 400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja zimetengenezwa nchini Canada na zitahudumia soko la ndani ndani na nchi za jirani zitakapoanza kazi.
Katibu Mkuu Uchukuzi,
Dkt. Leonard Chamriho akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa ATCL Mhandisi Ladislaus
Matindi pamoja na maafisa wengine wakiwa katika Ndege ya pili ya Bombadier Q400
iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) mara
ilipotua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa.
Katibu Mkuu Uchukuzi,
Dkt. Leonard Chamriho na viongozi wengine wakielekea kwenye Ndege ya pili ya
Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa
(ATCL) ilipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini
Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za
uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba
RAIS MAGUFULI AANZA KUWASHUGHULIKIA WANAOHUJUMU MISAADA KAGERA
Leo September 27 2016 taarifa
iliyotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim
Majaliwa muda mfupi baada ya kupokea hundi ya msaada wa Milioni
545 kutoka kwa Waziri Mkuu wa India imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua
uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Amantius Msole na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Steven Makonda.
Monday, 26 September 2016
ALIYOAGIZA LEO RAIS MAGUFULI BAADA YA KUFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BANDARINI JIJINI DSM

Leo September 26 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli ametembelea Bandari ya Dar es Salaam na kuzungumza na
wafanyakazi wa bandari hiyo ambapo pamoja na mambo mengine ametoa miezi miwili
kwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kununua mashine nne za kukagulia mizigo
bandarini (Scanning Mashine).
MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI YAMEZINDULIWA RASMI LEO MKOANI GEITA
naibu waziri wa mambo ya ndani Mhandisi Hamad Masauni azindua wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani, Kitaifa Mjini Geita leo
Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiyaangalia maandamano ya Wiki ya Nenda
kwa Usalama Barabarani.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani
nchini Mohamed Mpinga akizungumza katika Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa
Usalama Barabarani.
Washiriki wa maonyesho (waendesha bodaboda) wakiwa katika
maandamano ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani mjini Geita leo.
Maadhimisho
ya Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani
yamezinduliwa Rasmi leo Mkoani Geita katika viwanja vya Kalangalala na Naibu Waziri wa mambo ndani Mh.Ahamed Masauni,
huku ajali za waendesha piki piki maarufu boda boda zikiendelea kushika kasi kubwa zaidi nchini.
AFISA UVUVI NA MRATIBU ELIMU WAWEKWA CHINI YA ULINZI KWA MADAI YA KUTETEA UVUVI HARAMU
Afisa Uvuvi kata ya Nkome Merina Damian na Mratibu Elimu
Kata Thom Sharusanga wamewekwa chini ya ulinzi na Mkuu wa Wilaya ya Geita
Herman Kapufi baada ya kudaiwa kuhusika kuwatetea wavuvi haramu ambao wamekuwa
wakijihusisha kuvua samaki ambao hawaruhusiwa kwa kutumia nyavu haramu za
dududuu.
Hatua ya kusimamishwa imekuja
baada ya Mwenyekiti wa kitongoji Simon Kinasa kuanzisha operesheni na
kuwakamata baadhi ya watu wanaovua samaki chini ya kiwango ambapo baada ya
kuwakamata afisa uvuvi na Mratibu wakamuamuru awaachie wakidai mwenyekiti
amewakamata kwa madai amenyimwa rushwa.
Friday, 23 September 2016
MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI YA BUKOMBE MKOANI GEITA YAMHUKUMU MWALIMU KWA KOSA LA KUOMBA RUSHWA
RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ATUNUKIWA TUZO YA UONGOZI WA KISIASA NA UTETEZI
FAHAMU MECHI ATAKAZOZIKOSA LIONEL MESSI BAADA YA KUPATA JERAHA KATIKA MGUU WAKE(GROIN)
Usiku wa Septemba 21 Ligi
Kuu Hispania iliendelea kama kawaida kwa michezo
kadhaa kupigwa, lakini moja kati ya michezo iliyochezwa ni pamoja na mchezo
kati ya FC Barcelona dhidi ya Atletico Madrid uliomalizika kwa sare ya goli 1-1.
RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWINGINE LEO SEPTEMBER 23

Kufuatia hatua ya Serikali kununua hisa zote
za Bharti Airtel ambaye alikuwa mbia mwenza wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL)
na hivyo Serikali kumiliki hisa za Kampuni hiyo kwa asilimia 100, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Waziri
Waziri Kindamba kuwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.
Waziri Waziri Kindamba ameteuliwa kushika nafasi hiyo kuanzia leo
September 23 2016. Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa
TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura atapangiwa kazi nyingine.
Thursday, 22 September 2016
MAJINA YA WALIOFARIKI DUNIA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA BASI LA SUPER SHEM JIJINI MWANZA
Wednesday, 21 September 2016
M-PAWA KUTOKA VODACOM YAZIDI KUWATAJIRISHA WATANZANIA MSHINDI WA PILI APATIKANA

Meneja masoko Huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania ,Noel Mazoya
(katikati) akiongea na mmoja wa mshindi wa droo ya promosheni ya Jiongeza na
M-Pawa wakati wa hafla ya kuchezesha droo ya pili ya wiki iliyofanyika jijini
Dar es Salaam ambapo mkazi wa Arusha Isaack Pilemon alijishindia kitita cha
shilingi Milioni 20. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Meneja wa Huduma za M-Pawa
wa Benki ya CBA Eric Luyangi na Msimamizi wa bodi ya michezo ya Kubahatisha
nchini Bakari Maggid
RAIS MAGUFULI AIPONGEZA KILIMANJARO QUEENS KWA UBINGWA WA CECAFA CHALENJI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli, amewapongeza wachezaji wa Timu ya soka ya Wanawake ya
Tanzania Bara (Kilimanjaro Queens) kwa kuandika historia ya kuwa Mabingwa wa
kwanza wa Michuano ya kugombea kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki
na Kati (CECAFA Challenge) iliyofanyika katika Mji wa Jinja nchini Uganda.
WAZIRI NAPE NNAUYE AIPONGEZA KILIMANJARO QUEENS MABINGWA KOMBE LA CECAFA
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewapongeza Wachezaji wa
Kilimanjaro Queens kwa niaba ya serikali na kwa niaba ya watanzania kwa kazi
nzuri waliyoifanya mpaka kuwa mabingwa wa kwanza wa Kombe la CECAFA kwa mpira
wa miguu kwa wanawake Afrika Mashariki na Kati.
PICHA:MKUU WA MKOA WA KAGERA AIPOKEA KILIMANJARO QUEENS. AWAPONGEZA KWA USHINDI



Mkuu wa Mkoa wa Kagera
Meja Generali Mstaafu Salim Kijuu akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa
Kilimanjaro mara baada ya kuwasilini Mkoani Kagera wakitokea nchini Uganda
kushiriki mashindano ya CECAFA kwa wanawake ambapo wameibuka mabingwa kwa mwaka
2016.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Generali Mstaafu Salim Kijuu akipokea
kikombe cha ubingwa wa CECAFA kwa wanawake kutoka kwa Nahodha wa Kilimanjaro
Queens Sophia Mwasikili.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Generali Mstaafu Salim Kijuu(kushoto)
akiinua juu kikombe cha ubingwa wa CECAFA kwa wanawake alichokipokea kutoka kwa
Nahodha wa Kilimanjaro Queens Sophia Mwasikili(kulia).

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Generali Mstaafu Salim Kijuu(kushoto) akipokea
Bendera ya Taifa kutoka kwa katibu wa Chama cha Mpira mkoani Kagera Bw. Salum
Chama mara baada ya Mabingwa wa CECAFA kwa wanawake Kilimanjaro Queens kuwasili
kutoka Nchini Uganda katikati ni Mwenyekiti wa Soka la wanawake Amina Karuma.
WATU WENGINE KADHAA WAUAWA KATIKA MAANDAMANO NCHINI CONGO DRC

Waandamanaji nchini Congo DRC
Watu wengine kadhaa wameuawa katika siku
ya pili ya machafuko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jana, huku makao
makuu ya vyama vitatu vya upinzani yakichomwa moto.
Hayo yamejiri katika wimbi jipya la makabiliano kati ya
polisi na wapinzani wa Rais wa nchi hiyo Joseph Kabila
PICHA: BASI LA SUPER SHEM LAPATA AJALI NA KUUA WATU 11 JIJINI MWANZA HII LEO
Basi la Super Shem linalofanya safari
za Mwanza kwenda Mbeya limepata ajari ya kugongana na hiace katika kijiji
cha Hungumalwa Mwanza na kusababisha vifo vya watu wanaodaiwa kufika 11
asubuhi hii.
Tuesday, 20 September 2016
RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA WAATHIRIKA WA AJALI MKOANI NJOMBE
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli ametuma
salamu za rambirambi kwa familia zilizopatwa na msiba kufuatia ajali ya basi la
kampuni ya New Force iliyotokea jana Sept 19, 2016 majira ya saa 2:00 usiku katika
kijiji cha Lilombwi, kata ya Kifanya mkoani Njombe.
UTEUZI MWINGINE WA RAIS MAGUFULI LEO SEPTEMBER 20 2016
WAZIRI MKUU APOKEA MCHANGO WA WATUMISHI WA SERIKALI WA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amepokea jumla
ya sh. bilioni 1.040 kutoka kwa watumishi na wadau mbalimbali zikiwa ni misaada
kwa wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera
Septemba 10, mwaka huu.
TIMU YA SOKA YA WANAWAKE(KILIMANJARO QEENS) WATWAA KOMBE LA CECAFA CHALLENGE

Timu ya soka ya wanawake ya Tanzania Bara (The Kilimanjaro Qeens) imetwaa kombe la Challenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, baada ya kuifunga Kenya, mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliopigwa leo Jinja , nchini Uganda.
Kwa matokeo hayo, Kilimanjaro Qeens wanakuwa ndiyo
mabingwa wa kwanza na wa kihistoria wa michuano hiyo ambayo ni mipya kabisa
kuanzishwa katika ukanda ukanda wa Afrika Mashariki chini ya baraza lake la
CECAFA.
PICHA:MOJA YA NDEGE MPYA ZA ATCL ZILIZONUNULIWA NA SERIKALI YAWASILI NCHINI HII LEO

Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na
serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016.
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na Mkurugenzi wa
Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu, na maofisa wengine
wakisubiri kuwasili kwa Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na
serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo Septemba 20, 2016



Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na
serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikipata saluti ya maji
(Water Canon Salutation) toka kwa magari ya Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mara tu
bada ya kuwasili katika uwanja wa ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa sita
na robo juu alama leo Septemba 20, 2016


Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akisalimiana na
Rubani aliyerusha Ndege mpya moja kati ya mbili zilizonunuliwa na
serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016.


Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na Mkurugenzi wa
Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu, na maofisa wengine
wakiwa kwenye Moja ya Ndege mpya
mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL)
mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo
Septemba 20, 2016



Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akipeana mikono
kwa furaha na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw.
Pardeep Sandhu mara baada ya Moja ya Ndege mpya
mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL)
kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo Septemba 20, 2016,
Wengine ni marubani wa ndege hiyo
Subscribe to:
Posts (Atom)