Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati alipowasili
kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kuzindua Maadhisho ya Wiki ya Mazingira, Mei 31,
2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es salaam, Kate Kamba wakati
alipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam kuzindua Wiki
ya Mazingira, Mei 31, 2018. Wapili kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii,
Dkt. Hamisi Kigwangalla na watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani , Mhandisi
Evarest Ndikilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo
kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Space Engineering Limited, Bw.
Philip Mtui kuhusu mkaa uliotengenezwa kutokana na takataka na kufungashwa
kwenye kiroba tayari kwa kuuzwa wakati alipotembelea banda la Kampuni hiyo
kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar
es salaam, Mei 31, 2018. katikati ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi, Evarest Ndikilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata
maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Space
Engineering Limited, Bw. Philip Mtui kuhusu mkaa uliotengenezwa kutoka na
takataka na kufungashwa kwenye kiroba tayari kwa kuuzwa wakati alipotembelea
banda la Kampuni hiyo kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa
Pwani Mhandisi, Evarest Ndikilo na kushoto ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo,
Neema Matemba.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata Maelezo kutoka kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Edosama Hardware Limited, Edward Maduhu kuhusu bidhaa
mbalimbali zinazotokana na miti ambazo zinatengenezwa na kampuni hiyo wakati
alipotembelea mabada ya maonyesho kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye
Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Mei 31, 2018. Kulia ni Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Bibi
Nimwagile Mwaijumba wakati alipotembelea banda la Kituo cha Utengenezaji magari
cha Nyumbu na kujionea mashine ya kutengeneza mkaa bora kwa kutumia
takataka iliyobuniwa na kutengenezwa na kituo hicho. Waziri Mkuu alitembelea
mabanda ya maonyesho kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye viwanja
vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. Watatu kulia ni Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba na wapili
kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Opwani Mhandisi, Evarest Ndikilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza
Mkurugenzi wa Kampuni ya JHS , David Mwendapole wakati alipotoa maelezo
kuhusu majiko makubwa yanayotumia gesi kidogo katika maonyesho ya
Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31,
2018. Wanne kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na
Mazingira, January Makamba.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Wiki ya Mazingira
kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Mei 31, 2018.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika
maadhimisho ya wiki ya Mazingira wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
wakati alipowahutubia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei
31, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi
baada ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar
es salaam, Mei 30, 2018. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi
Evarest Ndikilo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangala,
Mwenyekiti wa CC wa Mkoa wa Dar es alaam, Kate Kamba,Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,
Kisare Matiku Makori na kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,
Muungano na Mazingira, January Makamba.