Tuesday 30 January 2018

SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA AGPAHI LAWAKUTANISHA WAVIU WASHAURI MKOA WA GEITA

DSC_1660
Baadhi ya washiriki wa  Warsha hiyo  wakiwa katika  kwenye ukumbi wa hotel ya Alphendo Mjini Geita wakati wa warsha ya kuwajengea uwezo wa watu wanaishi na VVU (WAVIU).

DSC_1685
Mwezeshaji katika warsha hiyo Bi.Anastella Stephen ambaye ni mratibu wa huduma za VVU na UKIMWI ngazi ya Jamii Wilayani Chato akisisitiza   WAVIU kuacha kuingilia majukumu ambayo  si ya kwao kama kutoa dawa kwa watu ambao wanavirusi vya ukimwi.

DSC_1677
Washiriki wa warsha wakiendelea na warsha ambayo imeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative( AGPAHI)  kwa kushirikiana na Halmashauri za wilaya ya Geita Vijijini,Geita Mji ,Chato na Bukombe.(Picha na Joel Maduka.)


DSC_1795
Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Richard Kambarangwe  akielezea umuhimu wa washiriki wa warsha hiyo kuunda vikundi ambavyo vitaweza kuwasaidia kuelimishana na pia  kufanya shughuli za ujasiliamali.

DSC_1699
Kulia ni Bw.Shilambele Mussa na Bi.Magdalena  Ngwada wakifanya maigizo ya namna ambavyo mhudumu anaweza kutoa huduma kwa  mtu mwenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi .

DSC_1706
MVIU mshauri  Bi.Imelda Assey kutoka CTC  ya hospitali ya wilaya ya  Chato akisisitiza  kuachana na dhana ya kuendelea kujinyanyapaa  kwa watu wanaishi na VVU.

DSC_1726
Mwezeshaji katika warsha hiyo Bi.Amida Yindi  ambaye ni Mratibu wa VVU na UKIMWI  ngazi ya jamii kwenye halmashauri ya wilaya ya Geita akitoa elimu ya namna WAVIU  wanatakiwa kuhakikisha mazingira wanafanyia kazi yanakuwa safi.

DSC_1770
Washiriki wakiwa kwenye vikundi wakijadili baadhi ya maswali.

DSC_1787


DSC_1693
Mwezeshaji  Bi.Amida Yindi akielekeza namna ambavyo MVIU mshauri anaweza kumhudumia mteja.

Na Joel Maduka,Geita.

Shirika  lisilo la kiserikali  la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI kwa kushirikiana na   Halmashauri za wilaya ya Geita Vijijini,Geita Mji ,Chato na Bukombe limewakutanisha  watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi  (WAVIU Washauri)kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutoa elimu  na kuwaunganisha wateja kutoka kwenye jamii kwenda kwenye vituo vya tiba na matunzo(CTC).

Warsha hiyo ambayo ilianza tarehe 29 January na inatarajia kumaliza tarehe 31january 2018 inafanyika kwenye ukumbi wa hotel ya Alphendo mjini Geita  ikiwashirikisha washiriki 46 kutoka kwenye Halmashauri nne zilizopo Mkoani humo.

Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Richard Kambarangwe  akizungumza wakati  warsha hiyo amesisitiza kwa WAVIU  washauri kuunda vikundi kwenye CTC zao  vya watu ambao wanaishi na virusi vya Ukimwi  ambavyo vitawasaidia kujiendeleza kwenye shughuli za ujasiliamali pamoja na kushauriana katika matumizi ya dawa za kufubaza makali ya VVU.

Kambarangwe ameeleza kuwa,kumeendelea kuwepo na tatizo kubwa la unyanyapaa kwa watu wanaoishi na VVU hivyo kupitia warsha  hii wamekuwa wakifanya jitihada za kutoa elimu kwenye jamii kwa kupitia WAVIU washauri  ili kuondokana na dhana ya unyanyapaa.

Mmoja kati ya watu ambao wanaishi na VVU kwa muda wa miaka  15, Bw. Eliya Malaki ambaye alipima VVU mwaka 2000 na kugundulika kuwa na maambukizi   alisema "bado kuna watu katika jamii hawaamini kuwa wamepata maambukizi ya VVU matokeo yake wanakimbilia kwa waganga wa jadi na wengine wamekuwa wakijinyanyapaa wenyewe kwa kushindwa kufika kwenye vituo vya tiba na matuzo hili kupata ushauri na saa".

MVIU mshauri wa Bi. Imelda Assey kutoka CTC ya hospitali ya  wilaya ya Chato alisema "kupitia warsha ambayo imefanywa na shirika la AGPAHI ni moja kati ya fursa ambayo itamsaidia kuendelea kutoa elimu zaidi kwa watu ambao wanaishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi,huku akisisitiza jamii ya watu ambao wanaishi na maambukizi kuachana na dhana ya kujinyanyapa bali kuikubali hali hiyo na kuzingatia ushauri ambao wanapewa na wataalamu wa afya ".

Mwezeshaji katika warsha hiyo Bi,Amida Yindi  ambaye ni mratibu wa VVU na UKIMWI  ngazi ya jamii kwenye halmashauri ya wilaya ya Geita,amewasisitiza WAVIU  washauri kujenga desturi ya kufanya usafi kwenye vituo ambavyo wanafanyia kazi pamoja na kuangalia kadi za wateja kama zimekusanywa na kuwekwa mahali ambapo  ni sahihi.


No comments:

Post a Comment