Tuesday 9 January 2018

WASICHANA WAONGOZA KWA UFAULU KIDATO CHA PILI NA DARASA LA SABA





Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA),Dk Charles Msonde ametangaza matokeo ya upimaji wa kitaifa kwa wanafunzi wa kidato cha pili na darasa la nne huku wasichana wakiongoza (waking’ara).
Akizungumzia matokeo ya kidato cha pili, Dkt. Msonde alisema wanafunzi 433,453 ambao ni asilimia 89.32 wamepata ujuzi na maarifa ya kuwawezesha kuendelea na Kidato cha Tatu. Kati ya hayo wasichana ni 224,736 ambao ni asilimia 88.55 na wavulana ni 208,717 ambao ni asilimia 90.17.

Kwa upande wa kidato cha pili, wasichana wameshika nafasi zote 10 bora kutoka kwenye shule tatu za Feza Girls, Canossa na Precious Blood. Kwa darasa la nne, wasichana wameshika nafasi nane za juu na wavulana wakishika nafasi ya tisa na 10. Katika matokeo ya mwaka 2016, wasichana walikuwa wanane na wawili wavulana, na mwaka 2015 wavulana walikuwa watano na wasichana watano.

Aidha, Msonde alisema wanafunzi 51.807 ambao ni asilimia 10.68 wamefeli kwa kushindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu. Mwaka 2016 wanafunzi 372,228 (asilimia 9.02) waliendelea na kidato cha tatu huku wanafunzi huku asilimia 8.98 ambao ni wanafunzi 36,737 walifeli.

“Somo ambalo wanafunzi wamefaulu zaidi ni Kiswahili kwa asilimia 91.92 na lile la ufaulu wa chini ni Hisabati yenye asilimia 32,”
alisema.
Akizitaja shule 10 zilizofanya vizuri kuwa ni Kemebos (Kagera), Canossa (Dar), St. Francis Girls (Mbeya), Marian Boys (Pwani), Kilimanjaro Islamic na Precious Blood (Arusha), St Augustine-Tagaste (Dar), Don Bosco Seminary (Iringa), Marian Girls (Pwani na Anwarite Girls (Kilimanjaro).

No comments:

Post a Comment